• HABARI MPYA

    Saturday, October 01, 2016

    SIMBA PUNGUFU WAIKATALIA YANGA, SARE 1-1, MASHABIKI WAVUNJA VITI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WATANI wa jadi, Simba na Yanga wamegawana pointi baada ya kutoa sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Ushindi unazidi kupandisha kileleni Simba SC ikifikisha pointi 17, baada ya kucheza mechi saba, wakati Yanga inatimiza pointi 11 baada ya kucheza mechi sita.
    Katika mchezo wa leo Yanga walitangulia kwa bao la Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe kabla ya mzalendo, Shizza Ramadhani Kichuya kuisawazishia Simba SC iliyocheza pungufu kwa muda mrefu baada ya Jonas Mkude kutolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza.
    Shizza Kichuya (katikati) akishangilia kwa kuonyesha ishara ya kidole kimoja cha kila mkono juu baada ya kuisawazishia Simba ikitoa sare ya 1-1 na Yanga
    Amissi Tambwe akishangilia baada ya kuifungia Yanga bao la kuongoza 

    Winga wa Simba, Shizza Kichuya (kushoto) akimtoka mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe
    Viungo Juma Mahadhi wa Yanga (kushoto) na Muzamil Yassin (kulia) wakipambana leo

    Tambwe alifunga bao lake dakika ya 26, akimalizia pasi ndefu ya beki Mbuyu Twite na kugeuka mbele ya beki wa Simba, Novat Lufunga kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Vincent Angban.
    Bao hilo lilizua kizaazaa, wachezaji wa Simba wakimvaa refa Martin Saanya wakidai mfungaji, Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga.
    Katika vurugu hizo, Saanya akamtoa kwa kadi nyekundu Nahodha wa Simba SC, Jonas Mkude dakika ya 29 kwa sababu ndiye aliyekuwa mstari wa mbele.
    Na mchezo ukasimama kwa takriban dakika tano baada ya mashabiki wa Simba kuanza kufanya vurugu waking’oa viti na kutupa uwanjani.
    Polisi walitumia milipuko kuwatuliza mashabiki hao na mchezo ukaendelea.



    Kipindi cha pili, Simba SC walibadlika pamoja na kucheza nguvu wakafanikiwa kupata bao la kusawazisha lililofungwa na winga Shizza Kichuyaa dakika ya 87 baada ya kona aliyochonga kuingia moja kwa moja nyavuni. 
    Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa 'Barthez',Juma Abdul,Mwinyi Hajji, Kevin Yondan/Andrew Vincent dk46, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Juma Mahadhi/Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amisi Tambwe, Donald Ngoma na Deus Kaseke/Haruna Niyonzima.
    Simba SC; Vincent Angban, Janvier Besala Bokungu, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Novart Lufunga/Juuko, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shizza Kichuya, Muzamil Yassim, Laudit Mavugo/Blagnon, Ibrahim Hajib/Mohamed ‘Mo’ Ibrahim na Mwinyi Kazimoto.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA PUNGUFU WAIKATALIA YANGA, SARE 1-1, MASHABIKI WAVUNJA VITI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top