• HABARI MPYA

  Saturday, October 01, 2016

  KULE MAVUGO NA HAJIB, HUKU TAMBWE NA NGOMA...PATAMU TAIFA LEO!

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KAMA ilifyotarajiwa, washambuliaji Ibrahim Hajib na Mrundi Laudit Mavugo wameanzishwa pamoja katika pambano dhidi ya mahasimu, Yanga jioni ya leo.
  Simba na Yanga zinamenyana jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na kocha Omog amewaanziwha pamoja wapachika mabao wake tegemeo, Hajib na Mavugo.
  Upande wake Yanga nako, kama kawaida kocha Mholanzi Hans van der Pluijm amewaanzisha pamoja Mrundi Amisi Tambwe na Mzimbabwe, Donald Ngoma.
  Kikosi kamili cha Simba SC; Vincent Angban, Janvier Besala Bokungu, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Novart Lufunga, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shizza Kichuya, Muzamil Yassim, Laudit Mavugo, Ibrahim Hajib na Mwinyi Kazimoto.
  Katika benchi watakuwapo Peter Manyika, Abdi Banda, Juuko Murshid, Said Ndemla, Mohamed Ibrahim, Frederic Blagnon na Jamal Mnyate.
  Juu; Kikosi cha Yanga na chini ni baadhi ya wachezaji wa Simba

  Kikosi cha Yanga SC; Ally Mustafa 'Barthez',Juma Abdul,Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Juma Mahadhi, Thabani Kamusoko, Amisi Tambwe, Donald Ngoma na Deus Kaseke.
  Katika benchi watakuwapo Deogratius Munishi 'Dida', Andrew Vincent 'Dante', Nadir Haroub 'Cannavaro', Oscar Joshua, Simoni Msuva, Obrey Chirwa na Haruna Niyonzima.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KULE MAVUGO NA HAJIB, HUKU TAMBWE NA NGOMA...PATAMU TAIFA LEO! Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top