• HABARI MPYA

    Sunday, October 02, 2016

    OKWI ATEMWA, KIIZA APETA KIKOSI CHA UGANDA THE CRANES

    KOCHA wa Uganda, The Cranes, Milutin Sredojevic 'Micho' ametaja orodha ya mwisho ya wachezaji 19 watakaomenyana na Togo mjini Lome Oktoba 4, mwaka huu katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, akimtema mshambuliaji wa zamani wa Simba na Yanga, Emmanuel Okwi.
    Mserbia huyo, Micho amemchukua mshambuliaji mwingine wa zamani wa Simba na Yanga, Hamisi Kiiza 'Diego' katika kikosi hicho ambacho kitamenyana pia na Ghana Oktoba 7 katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia Urusi mjini Tamale.
    Emmanuel Okwi (kulia) ametemwa kikosi cha Uganda, wakati Hamisi Kiiza 'Diego' amebaki

    Kikosi kamili aklichoteua Micho kinaundwa na makipa; Onyango Denis, Jamal Salim na Ochan Benjamin
    Mabeki: Wadada Nicholas, Iguma Denis, Isinde Isaac, Juuko Murushid, Ochaya Joseph na Walusimbi Godfrey.
    Viungo: Wasswa Hassan, Kizito Geoffrey, Aucho Khalid, Mawejje Tony na Oloya Moses.
    Washambuliaji: Kizito Luwagga, Miya Faruku, Massa Geoffrey, Kiiza Hamis na Sentamu Yunus.
    Timu hiyo iliyofanya mazoezi kwa mara mbili jana na leo Uwanja wa Taifa wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda inatarajiwa kuondoka usiku wa leo kwa ndege ya Ethiopia.
    Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), Darius Mugoye atasafiri na timu hiyo kama Mkuu wa msafara na timu hiyo inaondoka baada ya kupewa Sh. Milioni 620 za Uganda na Rais wa Jamhuri ya nchi hiyo, Yoweri Kaguta Museveni kusaidia maandalizi dhidi ya Ghana.
    Rais Museveni alimpigia simu binafsi, Rais wa FUFA, Mhandisi Moses Magogo jana kumpa ujumbe huo auwasilishe kwa wachezaji kuelekea mechi hiyo ya nyumbani.
    Wachezaji wanaotarajiwa kusafiri kutoka Kampala ni Patrick Ochan, Wadada, Kizito Geoffrey, Ochaya, Wasswa, Aucho na Tony Mawejje.
    Denis Onyango atawasili kesho na kuunganisha ndege kwenda Lome, Togo. Sentamu na Luwagga wataungna na timu mjini Lome wakati wachezaji wengine wataungana na timu Addis Ababa usiku wa leo kuunganisha safari ya kwenda Lome.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OKWI ATEMWA, KIIZA APETA KIKOSI CHA UGANDA THE CRANES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top