• HABARI MPYA

    Wednesday, June 01, 2016

    YORKE: SITA TU WAKO SALAMA MBELE YA MOURINHO MAN UNITED

    MSHAMBULIAJI wa zamani wa Manchester United, Dwight Yorke amesema wachezaji sita tu wa sasa wa timu hiyo ndiyo wako salama mbele ya kocha mpya, Jose Mourinho kubaki Old Trafford.
    Mreno huyo amerithi mikoba ya Mholanzi, Louis van Gaal baada ya msimu huu na anatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi cha timu hiyo hususan baada ya kuripotiwa kupewa fungu la Pauni Milioni 200 za kusajili wachezaji wapya.
    Yorke, aliyekuwamo kwenye kikosi cha Man United kilichotwaa mataji matatu mwaka 1999, mawili ya England na moja la Ligi ya mabingwa, amewataja wachezaji hao kuwa ni David de Gea, Anthony Martial, Michael Rashford na Nahodha Wayne Rooney ndiyo wanaweza kubaki mbele ya kocha wa zamani wa Chelsea msimu ujao. 
    Dwight Yorke amesema wachezaji sita tu wa sasa wa timu hiyo ndiyo wako salama mbele ya Jose Mourinho 

    Akizungumza katika mahojiano maalum na 888sport, Yorke amesema: "Kila mmoja mmoja anaruka ruka, lakini ni tetesi tu kwenye vyombo vya habari. Tunafahamu fika juu ya (Juan) Mata na Jose na hilo halina mabadiliko,". 
    "Kuna wachezaji wachache ambao ni wa Manchester United lakini wapo huko,"ameongeza mkali huyo wa mabao wa zamani wa Mashetani Wekundu, enzi zake akicheza pamoja na Andy Cole.
    Mourinho (right), pictured with United chief Ed Woodward, is expected to make widespread changes 
    Mourinho (kulia), akiwa na Mtendaji Mkuu wa United, Ed Woodward, anatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa 

    "Wamecheza chini ya kiwango na hakuna aliye salama ukiondoa De Gea, Martial, Rashford na Rooney. Kila mmoja baina yao wataangalia juu ya mabega yao,".
    Katika hao wachezaji wanne, Yorke binafsi amevutiwa zaidi na mwanasoka wa kimataifa wa Ufaransa, Martial ambaye amemaliza msimu akiwa mfungaji bora wa klabu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YORKE: SITA TU WAKO SALAMA MBELE YA MOURINHO MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top