• HABARI MPYA

  Wednesday, June 22, 2016

  REAL MADRID YAMREJESHA RASMI MORATA KUTOKA JUVE

  KLABU ya Real Madrid imethibitisha itamsajili tena mshambuliaji Alvaro Morata kutoka Juventus.
  Morata aliondoka Real kwenda Juventus mwaka 2014, lakini vigogo hao wa Hispania sasa wameamua kumrejesha kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 arudi kufanya kazi Bernabeu.
  Taarifa ya klabu imesema: "Real Madrid imeitaarifu Juventus juu ya uamuzi wake kumnunua Alvaro Morata, ambaye atarejea klabuni kwa maandalizi ya msimu mpya kwa maagizo ya kocha Zinedine Zidane,".
  Alvaro Morata anatarajiwa kurejea Real Madrid ambako mshambuliaji huyon alicheza kwa miaka minne kabla ya kwenda Juventus  PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  REKODI ZA ALVARO MORATA  

  Real Madrid: 2010-2014
  Juventus: Tangu 2014-
  Jumla ya mechi: 228
  Jumla ya mabao: 83 
  Ada ya uhamisho ya Morata haijatangazwa, lakini taarifa zinasema kwamba inaweza kufika Pauni Milioni 23.
  Bado inasubiriwa kujulikana kama Morata atarejea kwa mabingwa hao wa Ulaya msimu ujao, au ataamua kwenda kujiunga na klabu nyingine za Ulaya zinazomtaka, zikiwemo za England.
  Mkurugenzi Mkuu wa Juve, Giuseppe Marotta mapema alisema kwamba mshambuliaji huyo ambaye ameichezea mechi zote za Euro 2016 hadi sasa na kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 Ijumaa dhidi ya Uturuki, anaweza kurejea nyumbani kwao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REAL MADRID YAMREJESHA RASMI MORATA KUTOKA JUVE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top