• HABARI MPYA

  Wednesday, June 08, 2016

  MWENYEKITI ALGERIA AFUNGIWA MAISHA KWA KUPANGA MATOKEO

  MWENYEKITI wa klabu ya Abdelmadjid Yahi wa US Chaouia ya Algeria amefungiwa maisha kujihusisha na soka jana baada ya kusema kwenye Televisheni upangaji matokeo ulikithiri naye pia alishiriki.
  Mwezi uliopita, Abdelmadjid Yahi wa US Chaouia alilalamikia kushuka kwa timu yake hadi Daraja la Tatu akisema kulitokana na upangaji matokeo wa wazi.

  Abdelmadjid Yahi amefungiwa maisha baada ya kukiri hadharani aliwahi kushiriki kupanga matokeo ya mechi

  Kisha akasema yeye mwenyewe aliwahi kushiriki upangaji wa matokeo ya mechi siku za nyuma.
  Yahi, ambaye amekuwa Mwenyekiti wa US Chaouia kwa karibu miaka 25, alishughulikiwa na mamlaka za soka jana kwa kufungiwa maisha kujihusisha na soka pamoja na ktozwa faini ya dinar 200,000 (sawa na dola za Kimarekani 1,825 au Euro 1,600).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWENYEKITI ALGERIA AFUNGIWA MAISHA KWA KUPANGA MATOKEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top