• HABARI MPYA

  Saturday, June 11, 2016

  MADAM RITA ALAMBA DILI AZAM TV

  Na Nurat Mahmoud, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya Azam TV kwa kushirikiana na BenchMark Production 360 imezindua kipindi chake kipya cha Rita Paulsen Show kitakachoanza kuruka Jumapili saa 1:00 Usiku kupitia channel ya AzamTWO inayopatikana kwenye vifurushi vyote vya AzamTV.
  Kaimu Mkurugenzi mkuu wa AzamTV Tido Mhando amesema kuwa kipindi hiki kimekuja wakati muafaka kikitoa majibu ya mpango mkakati ambao AzamTV imekuwa ikifanyia kazi maoni ya watazamaji wake kwa kuwaletea vipindi bora vinavyoelimisha, burudisha na vyenye maudhui yanayofaa kutazamwa na familia nzima.
  Naye mwasisi wa Bench Mark Production na Mtangazaji wa kipindi hicho Rita Paulsen ama maarufu kama Madam Rita alifunguka kwa kuelezea namna kipindi hicho kitakavyokuwa ni cha kipekee kwani kitabeba mijadala iliyofanyiwa uchambuzi wa kina na hadhi yake ni ya kimataifa na kitaifa na kitawafanya watazamaji wasibanduke hata kupepesa pembeni kuanzia mwanzo hadi mwisho kutokana na uhondo wake.
  Kutoka kulia Tido Mhando, Rota Poulsen na Mgope Kiwanga
  Rita Alisema kuwa ‘Safari yakufikia hapa haikuwa kazi rahisi hata kidogo kutokana na majaribu tuliyokutana nayo ya kuandaa kitu chenye ubora huu, na naweza kuthubutu kusema kuwa huyu ni ‘mtoto’ wa kipekee kwa Benchmark Production ambaye amekuwa akisukwa kuanzia mwaka 2007 na tumekuwa tukihaha kupata mahala sahihi ambapo wataweza kumnyanyua ‘mtoto’ huyu kwa hadhi yake anayostahili na hatimaye AzamTV pekee wameona umuhimu na thamani yake na kutupatia nafasi hii adhimu ya kufanya nao kazi ambapo leo tunakizindua rasmi’ 
  Lengo kuu la Rita Paulsen Show ni kuelimisha, kuburudisha na kugusa maisha ya watu na kurudisha Imani ya ubinadamu na matumaini ya maisha ambapo wageni mbalimbali wataalikwa wakiwemo watu maarufu, wenye historia ya pekee na hata wa kawaida watakaofunguka juu ya mapambano na visa vya maisha yao waliyopitia hadi kufikia kwenye mafanikio waliyonayo sasa.
  Tido nae aliongezea kuwa ‘kipindi hiki kitagusa hisia za watu kwani zitamuweka mtazamaji katika nafasi ile aliyokuwa nayo mhusika na kuelewa ni vipi na kwa nini alichukua maamuzi magumu, ya kuogofya ya kusikitisha n ahata kufurahisha pia yatakayowaacha midomo wazi,mioyo iliyoumia na macho yaliyojaa machozi kutokana na msisimko wake’
  Kama lilivyo jina la kipindi, Rita Paulsen ni mwanamke aliyetawala ulingo wa vipindi vya burudani kwa muda mrefu sasa na imekuwa ni ndoto yake kubwa kutumia nafasi yake na nguvu zake ndani ya nchi n ahata Afrika kuleta mabadiliko kwenye maisha ya watu, na kupitia chake hiki watazamaji wataweza kumuona kivingine akigusa maisha ya watu kiuchumi, kijamii,kiimani na hata kimwili na kuwarudishia Imani waliyopeteza juu ya maisha.
  Rita Paulsen Show ni kipindi cha dakika 45 kilichogawanyika katik asehemu kuu tatu, kitakaruka kila Jumapili saa 1:00 usiku na marudio ni Alhamis saa 12:00 Jioni kupitia channel ya AzamTWO ndani ya AzamTV pekee.
  Utashuhudia simulizi za nguvu za mwanamke aliyetelekezwa, watu maarufu wakifanya vitu ambavyo hukuvitegemea na kitakuacha na ile hisia ya kujisikia vizuri mwanzo mwisho
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MADAM RITA ALAMBA DILI AZAM TV Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top