• HABARI MPYA

  Monday, June 13, 2016

  KOCHA KABWE AREJEA POWER DYNAMOS BAADA YA 15

  KLABU ya Power Dynamos ya Zambia imemteua Danny Kabwe kuwa kocha wake mpya.
  Kocha huyo wa zamani wa Zanaco ametambulishwa Juni 11 Uwanja wa Arthur Davies mjini Kitwe na anajiunga na Power kwa Mkataba wa miaka mitatu na nusu.
  Hii ni mara ya pili kwa Kabwe kufanya kazi na Power baada ya awali kuwa na timu hiyo ya Kitwe miaka 15 iliyopita.
  "Kurejea kwangu huku ni zaidi ya imani kubwa waliyonayo Power na kujiamini kwao juu yangy na hiyo ndiyo sababu nimerudi, nimekuja kuwathibitishia binafsi,” amesema Kabwe.

  "Hata wakati ninaondoka, niliondoka vizuri na hata ninaporejea, nitaonyesha tofauti," amesema Kabwe anayechukua nafasi ya Tennant Chilumba aliyefukuzwa Mei 5 baada ya miaka mitatu ya kuwa kazini Power.
  Kocha huyo mpya wa Power anarejea Kitwe baada ya kuwaacha mabingwa mara sita wa Zambian katikati ya msimamo wa Ligi msimu wa 2001 na kuhamia Zanaco.
  Zanaco ilifurahia kazi ya Kabwe aliyewaongoza kutwaa taji lao la kwanza la Ligi Kuu ya FAZ mwaka 2002 na kulitetea mwaka 2003.
  Kabwe pia aliwahi kuwa Kocha Msaidizi wa Zambia kwa muda mwaka 2001 chini ya Jan Brouwer. Anaichukua Power ambayo kwa sasa inashika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi Kuu ya FAZ ikiwa na pointi 21, ikizidiwa saba na  vinara na mahasimu wao wa jadi, Nkana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA KABWE AREJEA POWER DYNAMOS BAADA YA 15 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top