• HABARI MPYA

  Saturday, June 11, 2016

  KAKOLANYA: NATARAJIA KUJIFUNZA MENGI KWA BARTHEZ, DIDA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KIPA mpya Yanga SC, Benno Kakolanya amesema kwamba anatarajia kujifunza mambo mengi kwa makipa wazoefu na bora kwa sasa nchini, Deo Munishi ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez’.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo, Kakolanya amesema kwamba anataka wafahamu hajaingia kugombea namba dhidi ya makipa hao.
  “Hawa ni makipa bora ambao ninahitaji kujifunza mengi kutoka kwao. Nataka watu wajue kwamba, sijaja Yanga kushindana nao, nimekuja kujifunza kutoka kwao,”amesema.
  Benno Kakolanya amesema kwamba anatarajia kujifunza mambo mengi kwa makipa wazoefu na bora kwa sasa nchini, Deo Munishi ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez’

  Kakolanya amesema kwamba nafasi ya kudaka Yanga itakuja kutokana na juhudi zake na wepesi wa kushika mafundisho ya mwalimu wa makipa, Juma Pondamali.
  “Wakati wote nipo Prisons, Dida na Barthez ndiyo walikuwa makipa wangu, hawa jamaa nawakubali sana, nimeanza kujifunza kutoka kwao tangu nipo Prisons na sasa nimepata wasaa mzuri baada ya kukutana nao hapa,”amesema. 
  Kakolanya mwenye umri wa miaka 22, amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na wafalme wa soka ya Tanzania, Yanga SC, akitokea timu ya Jeshi la Magereza Mbeya, Prisons iliyomuibua Mbaspo Academy.
  Kakolanya sasa anaungana na na makipa watatu waliopo Yanga, mbali na Dida na Barthez, mwingine ni Benedicto Tinocco kufanya idadi ya makipa wanne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAKOLANYA: NATARAJIA KUJIFUNZA MENGI KWA BARTHEZ, DIDA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top