• HABARI MPYA

  Saturday, June 11, 2016

  BEKI LA MWADUI LASAINI MIAKA MIWILI SIMBA SC

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imemsajili beki wa kati wa Mwadui FC ya Shinyanga, Emmanuel Semwanza (pichani kulia) kwa Mkataba wa miaka miwili.
  Semwanza ni kati ya mabeki waliofanya vizuri msimu ulioamlizika Mei wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ambaye alikuwa anawaniwa pia na Mbeya City.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo Semwanza amesema amesaini Mkataba wa miaka miwili na Simba SC baada ya kumaliza Mkataba wake na Simba SC.
  Simba SC bado haijatangaza mchezaji yeyote mpya iliyemsajili, lakini BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE inafahamu mbali na Semwanza pia iko mbioni ya kukamilisha usajili wa mchezaji mwingine wa Mwadui, kiungo Jamal Mnyate.
  Na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba usajili wao safari hii ni siri.
  “Siwezi kukuambia chochote, sisi tunafanya usajili wetu kwa siri. Na hivi ninavyokuambia tumekwishasajili wapya sita,”amesema Poppe.
  Semwanza (kushoto) akiwa na Paul Nonga ambaye Desemba mwaka jana alisajiliwa Yanga
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI LA MWADUI LASAINI MIAKA MIWILI SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top