• HABARI MPYA

  Saturday, June 04, 2016

  CAMEROON YAFUZU AFCON 2017 BAADA YA KUICHAPA 1-0 MAURITANIA UGENINI

  TIMU ya taifa ya Cameroon imekuwa nchi ya tatu kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2017 mbali ya wenyeji Gabon baada ya ushindi wa 1-0 Ijumaa dhidi ya Mauritania mjini Nouakchott.
  Simba Wasiofungika sasa wanaungana na Algeria, Morocco na wenyeji Gabon kujihakikishia nafasi ya kucheza AFCON ya mwakani.
  Kiungo Edgar Salli alifunga bao pekee dakika ya 29 kuihakikishia tiketi hiyo Cameroon.
  Cameroon sasa inafikisha pointi 11 kileleni mwa kundi M, ikiwazidi pointi nne Mauritania. Afrika Kusini ina pointi tatu huku Gambia inayoshika mkia ina pointi mbili.
  Gambia watakuwa wenyeji wa Afrika Kusini Jummosi mjini Bakau.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAMEROON YAFUZU AFCON 2017 BAADA YA KUICHAPA 1-0 MAURITANIA UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top