• HABARI MPYA

    Monday, June 13, 2016

    AFRICAN SPORTS YAPANGWA PAMOJA NA ABAJALO, ASHANTI ZAPANGWA MAKUNDI DARAJA LA KWANZA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU za Abajalo, Ashanti United za Dar es Salaam zimepangwa pamoja na African Sports ya Tanga katika Kundi Ligi Daraja la kwanza Tanzania Bara.
    Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetangaza makundi matatu ya timu zitakazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes msimu wa 2016/2017. Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Agosti, mwaka huu mara baada ya kukamilisha mchakato wa usajili unaoanza Juni 15, 2016.
    Kila Kundi lina timu nane na timu nyingine katika katika Kundi A ni Kiluvya United ya Pwani, Friends Rangers ya Dar es Salaam, Lipuli  ya Iringa, Mshikamano FC ya Dar es Salaam na Polisi Dar ya Dar es Salaam.
    African Sports imeporomoka msimu huu kutoka Ligi Kuu

    Kundi B lina timu za  JKT Mlale ya Ruvuma, Coastal Union ya Tanga, Kimondo FC ya Mbeya, Kinondoni Municipal Council ya Dar es Salaam, Kurugenzi ya Iringa, Mbeya Warriors ya Mbeya,. Njombe Mji  ya Njombe na Polisi Morogoro ya Morogoro.
    Kundi C lina timu za Alliance Schools ya Mwanza, Mgambo Shooting ya Tanga, Mvuvumwa FC ya    Kigoma,  Panone FC ya Kilimanjaro, Polisi Dodoma ya Dodoma, Polisi Mara ya Mara, Rhino Rangers ya Tabora na Singida United ya Singida.
    Wakati huo huo: Rais wa TFF, Jamal Malinzi amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha John Mabula - mchezaji wa zamani wa timu ya soka ya Mtibwa Sugar ya Morogoro inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Mbali ya Mtibwa Sugar, taarifa za Mabula ambaye pia amewahi kuchezea Moro United ya Morogoro na Shinyanga Shooting ya Shinyanya kwa mafanikio nafasi ya ulinzi kwa muda mrefu katika timu hizo, aliuawa kwa kuchomwa kisu na mwenzake alipokuwa akiamulia ugomvi huko Kitunda - nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
    Rais Jamal Malinzi amemwelezea Mabula kuwa ni mchezaji aliyekuwa na uwezo na uadilifu na mchango wake katika soka utabaki katika dhana ya kumbukumbu ya wachezaji mahiri wa Tanzania waliotokea kucheza nafasi ya ulinzi japokuwa ametangulia mbele za haki.
    Rais Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa uongozi wa timu ambazo alicheza ambazo ni Mtibwa Sugar, Moro United na Shinyanga Shooting; kadhalika familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki walioguswa na msiba huo wa gwiji huyo aliyepata pia kucheza timu ya taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ ya mwaka 2002-2004.
    Rais Malinzi amewaasa wadau wote kuwa watulivu wakati huu mgumu wa msiba wa mpendwa wetu Mabula hasa kutokana na mazingira ya kifo. Bwana alitoa, Bwana Ametwaa, Jina la Bwana lihimidiwe. Amina.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AFRICAN SPORTS YAPANGWA PAMOJA NA ABAJALO, ASHANTI ZAPANGWA MAKUNDI DARAJA LA KWANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top