• HABARI MPYA

  Friday, April 15, 2016

  LIVERPOOL JOGOO KWELI, YAING'OA DORTMUND ULAYA

  TIMU za Liverpool, Shakhtar Donetsk na Villarreal zimetinga Nusu Fainali ya michuano ya Europa League 2016 baada ya mechi za marudiano usiku wa Alhamisi. 
  Liverpool imesonga mbele baada ya kuifunga 4-3 Borussia Dortmund Uwanja wa Anfiled, hivyo kufuuz kwa ushindi wa jumla wa 5-4 baada ya wiki iliyopita kutoa sare ya 1-1 Ujerumani.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Divock Origi dakika ya 48, Philippe Coutinho dakika ya 66, Mamadou Sakho dakika ya 77 na Dejan Lovren dakika ya 90 na ushei, wakati ya Dortmund yamefungwa na Henrikh Mkhitaryan dakika ya tano, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya tisa na Marco Reus dakika ya 57.
  Dejan Lovren akienda hewani kuifungia bao la ushindi Liverpool dakika ya mwisho Uwanja wa Anfield PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Shakhtar Donetsk imeifunga 4-0 Sporting Braga na kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 6-1 baada ya awali kushinda 2-1 ugenini. Mabao ya Shakhtar yamefungwa na Darijo Srna kwa penalti dakika ya 25, Ricardo Jose Araujo Ferreira aliyejifunga dakika ya 42 na 73 na Viktor Kovalenko dakika ya 50 Uwanja wa Lviv.
  Villarreal imeshinda 4-2 ugenini dhidi ya Sparta Prague na kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 6-3, baada ya wiki iliyopita kushinda 2-1 nyumbani.
  Sevilla imeing’pa Athletic Club ka penalti 5-4 kufuatia sare ya jumla ya 3-3, baada ya kila timu kushinda 2-1 mechi ya nyumbani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL JOGOO KWELI, YAING'OA DORTMUND ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top