• HABARI MPYA

    Thursday, October 03, 2019

    MOLINGA AFUNGA MABAO MAWILI NA KUINUSURU YANGA KUCHAPWA NA POLISI, YATOA SARE 3-3

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    YANGA SC imenusurika kupoteza mchezo wa pili mfululizo katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kulazimisha sare ya 3-3 na Polisi Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
    Mshambuliaji mpya, kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), David Molinga ‘Falcao’ ndiye aliyeinusuru Yanga na fedheha leo baada ya kufunga mabao mawili kipindi cha pili timu ikitoka nyuma kwa 3-1 na kupata sare ya 3-3.  
    Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Abdallah Mwinyimkuu, alyesaidiwa na Makame Mdogo na Joseph Pombe, Yanga walitangulia kupata bao kupitia kwa kiungo wake mshambuliaji mkongwe, Mrisho Khalfan Ngassa.


    Mshambuliaji Ditram Nchimbi anayecheza kwa mkopo kutoka Azam FC akafunga mabao matatu mfululizo kuanzia dakika ya 29, 55 na 58 kuipa uongozi timu ya kocha Suleiman Matola katika mchezo wa ugenini.
    Hata hivyo, Molinga aliye katika msimu wake wa kwanza akafunga kwa kchwa dakika ya 22 akimalizia krosi kutoka kulia na klwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 65 kuitoa nyuma Yanga na kufanya mechi iwe 3-3.
    Polisi Tanzania wakamalizia dakika tano za majeruhi wakiwa pungufu ya mchezaji ya mmoja kufuatia Yassin Mustafa kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 90.
    Leo Yanga ilicheza bila kocha wake, Mkongo Mwinyi Zahera ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu kufuatia tuhuma za kutoa maneno yasiyofaa baada ya mechi ya kwanza wakifungwa 1-0 na Ruvu Shooting Agosti 28 hapo hapo Uwanja wa Uhuru. 
    Timu iliongozwa na Kocha Msaidizi, Mzambia Noel Mwandila aliyekuwa akisaidiwa na kocha wa makipa, Manyika Peter. 
    Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata, Juma Abdul, Ally Mtoni ‘Sonso’, Kelvin Yondan, Lamine Moro, Abdulaziz Makame, Mrisho Ngassa, Feisal Salum ‘Fei Toto’, David Molinga, Juma Balinya/Mapinduzi Balama dk46 na Sadney Urikhob/Deus Kaseke dk46.
    Polisi Tanzania; Kulwa Manzi, William Lucian ‘Gallas’, Yassin Mustafa, Pato Ngonyani, Iddi Mobby, Baraka Majogoro, Andrew Chamumu, Hassan Maulid, Ditram Nchimbi, Marcel Kaheza na Sixtus Sabilo/Mohamed Mkopi dk70.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MOLINGA AFUNGA MABAO MAWILI NA KUINUSURU YANGA KUCHAPWA NA POLISI, YATOA SARE 3-3 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top