• HABARI MPYA

    Thursday, October 03, 2019

    KAPOMBE AREJESHWA KIKOSINI TAIFA STARS, NDAYIRAGIJE AENDELEA KUMCHUNIA AISHI MANULA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mrundi wa timu ya taifa ya Tanzania, Etienne Ndayiragije amemrejesha kikosini beki Shomari Kapombe kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji, Rwanda mjini Kigali Oktoba 14.
    Lakini Ndayiragije ameendelea ‘kumkaushia’ kipa bora nchi, Aishi Salum Manula wa Simba SC, akiwachukua tena Juma Kaseja wa KMC, Metacha Mnata wa Yanga SC Said Kipao wa Kagera Sugar.
    Mchezo dhidi ya Rwanda ni maandalizi ya mchezo wa marudiano wa kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya Sudan utakaochezwa Oktoba 18 nchini Uganda.
    Mechi ya kwanza Taifa Stars ilifungwa 1-0 nyumbani Dar es Salaam na natakiwa kwenda kushinda 2-0 ugenini ili kukata tiketi ya kucheza fainali za michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee. 
    Kikosi kamili cha Taifa Stars kwa ajili ya mchezo dhidi ya Rwanda ambacho kitamenyana pia na Sudan kinaundwa na makipa; Juma Kaseja (KMC), Metacha Mnata (Yanga SC) na Said Kipao (Kagera Sugar).
    Mabeki; Salum Kimenya (Tanzania Prisons), Shomari Kapombe (Simba SC), Gardiel Michael (Simba SC), Mohammed Hussein (Simba SC), Kelvin Yondan (Yanga SC), Erasto Nyoni (Simba SC), Bakari Mwamnyeto (Coastal Union).
    Viungo; Himid Mao (ENPPI/Misri), Jonas Mkude (Simba SC), Farid Mussa (Tenerife/Hispania), Adi Yussuf (Solihull Moors/England), Iddi Suleiman ‘Nado’ (Azam FC), Mudathir Yahya (Azam FC), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Muzamil Yassin (Simba SC), Abdulaziz Makame (Yanga SC), Feisal Salum (Yanga SC) na Simon Msuva (Difaa Hassan El-Jadidi/Morocco)  
    Washambuliaji; Kelvin John (Huru), Shaaban Iddi Chilunda (Azam FC), Ayoub Lyanga (Coastal Union), Andrew Simchimba (Azam FC), Miraj Athumani (Simba SC) na Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk). 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAPOMBE AREJESHWA KIKOSINI TAIFA STARS, NDAYIRAGIJE AENDELEA KUMCHUNIA AISHI MANULA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top