• HABARI MPYA

    Sunday, August 04, 2019

    TAIFA STARS YAITUPA NJE HARAMBEE KWA MATUTA KUFUZU CHAN 2020

    Na Mwandishi Wetu, NAIROBI
    TANZANIA imefanikiwa kutinga hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) baada ya ushindi wa penalti 4-1 dhidi ya Kenya jioni ya leo Uwanja wa Moi Kasarani mjini Nairobi, Kenya.
    Shujaa wa Taifa Stars leo alikuwa ni kipa mkongwe, Juma Kaseja aliyerejeshwa kikosini baada ya miaka sita ambaye aliokoa penalti ya Michael Kibwage.
    Waliofunga penalti za Tanzania ni mabeki Erasto Nyoni, Paul Godfrey ‘Boxer’, Gardiel Michael na mshambuliaji Salum Aiyee.

    Mshambuliaji wa Tanzania, Idd Suleiman 'Nado' akimtoka mchezanji wa Kenya, Kenneth Muguna leo Nairobi

    Kenya walipata penalti moja tu, ambayo ilifungwa na Cliffton Miheso Ayisi, huku nyingine wakikosa Michael Kibwage na Joash Achieng Onyango.
    Sasa Tanzania itakutana na Sudan katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya CHAN ya mwakani nchini Cameroon, mechi ya kwanza ikichezwa Dar es Salaam Septemba 20 na marudiano Oktoba 18 Khartoum.
    Kikosi cha Kenya kilikuwa; John Oyemba, Philemon Otieno/Ibrahim Shambi, Clifton Miheso, Mike Kibwage, Joash Onyango, Dennis Odhiambo, Samuel Onyango, Kenneth Muguna, Sydney Lokale/Enosh Ochieng, Whyvone Isuza na Duke Abuya/ David Owino.
    Tanzania; Juma Kaseja, Paul Godfrey, Gardiel Michael, Erasto Nyoni, Kelvin Yondan, Jonas Mkude, Frank Domayo/Salim Aiyee, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco/Ayoub Lyanga, Iddi Suleiman ‘Nado’ na Hassan Dilunga/Abdulaziz Makame.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS YAITUPA NJE HARAMBEE KWA MATUTA KUFUZU CHAN 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top