• HABARI MPYA

    Friday, August 09, 2019

    TAIFA STARS KUMENYANA NA BURUNDI KUWANIA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA QATAR 2022

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TANZANIA itamenyana na Burundi katika hatua ya awali kuwania kupangwawa kwenye makundi ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.
    Kwa mujibu wa ratiba iliyotoka leo, mechi ya kwanza baina ya Taifa Stars na Int’hamba Murugamba itachezwa Uwanja wa Taifa mjini Bujumbura Septemba 2 kabla ya timu hizo kurudiana Septemba 10 mjini Dar es Salaam. 
    Mechi nyingine Ethiopia itamenyana na Lesotho, Somalia na Zimbabwe, Eritrea na Namibia, Djibouti na Eswatini, Botswana na Malawi, Gambia na Angola na Liberia dhidi ya Sierra Leone.

    Nao Mauritius watamenyana na Msumbiji, Sao Tome na Principe dhidi ya Guinea-Bissau, Sudan Kusini na Equatorial Guinea, Comoro na Togo, Chad na Sudan na Shelisheli dhidi ya Rwanda.
    Washindi 14 wa jumla wataungana na timu nyingine 26 za viwango vya juu barani, wakiwemo majirani Kenya na Uganda kugawanywa kwenye makundi 10 ya timu tano kila moja kuanza rasmi kuwania tiketi ya Qatar 2022.
    Washindi wa makundi yote wataingia hatua ya tatu na ya mwisho ya mwisho ya mbio hizo za Qatar. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAIFA STARS KUMENYANA NA BURUNDI KUWANIA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA QATAR 2022 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top