• HABARI MPYA

  Sunday, August 04, 2019

  OSIAN ROBERT ATEULIWA KUWA MKURUGENZI MPYA WA UFUNDI MOROCCO

  SHIRIKISHO la Soka Morocco (FRMF) limemteua Kocha Msaidizi wa zamani wa Wales, Osian Robert kuwa Mkurugenzi wake mpya wa Ufundi.
  Mtaalamu huyo mwenye umri wa miaka 54 amesaini mkataba wa miaka mitano ambao utaanza Septemba atakapoachia majukumu ya Ukocha Msaidizi wa Wales. 
  Anachukua nafasi ya Mmorocco, Nasser Larguet ambaye amekuwa akiutumikia wadhifa huo kuanzia mwaka 2014 hadi mapema 2019.
  Roberts aliibukia kwenye kikosi cha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 16 cha Wales (U16) kabla ya kupandishwa U18 na baadaye kufundisha Porthmadog katika Ligi Kuu ya Wales mwaka 1999.

  Mwaka 2007 ndipo akawa Kocha Msaidizi wa Wales chini ya Gary Speed, Chris Coleman na kocha wa sasa, Ryan Giggs. 
  Akiwa mmoja wa watu wenye ushawishi kwenye soka ya Wales siku za karibuni, Osian Roberts alitoa mchango mkubwa kwa nchi yake kufuzu Euro 2016 na mafanikio ya mchezaji mwenzake,  Gareth Bale.
  Katika hatua nyingine, Houcine Ammouta, aliyeiongoza Wydad Athetic Club kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2017 ameteliuwa kuwa kocha wa kikosi cha wachezaji wa nyumbani wa Morocco, ambacho kitawania tiketi ya CHAN 2020.
  Jamal Sellami, aliyeshinda taji CHAN mwaka 2018 katika fainali zilizofanyika nyumbani amethibitishwa kuwa kocha wa U-20 na Mfaransa, Patrice Beaumelle atakuwa kocha wa U-23.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OSIAN ROBERT ATEULIWA KUWA MKURUGENZI MPYA WA UFUNDI MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top