• HABARI MPYA

  Monday, August 05, 2019

  NAOMBA NIONGEE NANYI BAADA YA WIKI YA MWANANCHI KUPITA

  Na Dominick Salamba, DAR ES SALAAM
  KATIKA hali isiyotarajiwa na pengine kuonekana ni mshangao wa wengi kuanzia wale waliokuwa majumbani hata wale ambao walifika uwanjani nazungumzia uwanja wa Taifa kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi ambapo klabu ya Yanga SC ilikuwa ikitamatisha wiki ya hamasa na mambo mbalimbali yaliyofanyika nchi nzima na mwishowe kumalizia katika uwanja wa Taifa,Ilikuwa ni historia mpya kwa klabu hiyo kongwe umati mkubwa wa watu ulijieleza kwa namna wapenzi wa soka walivyo na shauku na timu yao..Sikushangaa nilipoongea na kipa wa Kariobang sharks na alipokiri kuwa kule kwao Kenya huwezi kuta kitu kama hiki na hata umati ule hakuamini kuwa ni mashabiki wa timu moja na kwenda mbali na kusema Tanzania mna bahati ya kupata mashabiki wapenda soka kama hawa.

  Nikianza na hili la umati na hamasa kubwa kiasi kile kwanza nianze kuwapongeza kamati ya utendaji chini ya mwenyekiti Dr. Msolwa pamoja na kamati ya hamasa ambayo imeongozwa vema na mwenyekiti wake Mh.Antony Mavunde pamoja na katibu wake Bwana Deo Mutta pamoja na wajumbe wote kiukweli walifanya kazi kubwa sana hadi kufikia kilele cha kufana kiasi kile,kwani wameweza kuwaunganisha mashabiki wa Yanga nchi nzima mikoa karibu yote ilileta wawakilishi nilipata bahati kuona vikundi vya mashabiki kutoka Geita, Mbeya, Iringa, Morogoro, Tanga, Dodoma na mikoa mingine jambo ambalo limefanyika kwa hiari na hamasa kubwa.
  Lakini pia mpangilio wa kuingia uwanjani,upatikanaji wa tiketi na taratibu zingine walijitahidi sana kufanikisha kwa kiasi kikubwa sana jambo ambalo ni la kupongezwa ingawa pongezi kubwa ziende kwa mashabiki ambao walijitoa sana na kufanikisha zoezi hilo kubwa la kihistoria..
  Mapungufu hayakosekani kwani ni sehemu ya ubinadamu na kwakuwa ni mwanza nadhani yatarekebishwa ili kulifanya tukio hili kuzidi kufanikiwa mwaka hadi mwaka ili iwe ni miongoni mwa SIKUKUU  nchi nzima. hongereni sana wote mlioshiriki kwa namna moja au nyingine.
  Tuje kwa upande wa timu  ambayo ndio ilikuwa sababu ya umati wote kama ifuatavyo.

  USAJILI
  Jana nimepata nafasi ya kuwashuhudia wachezaji waliosajiliwa na kupata nafasi ya kucheza ingawa niliwaona wakiwa mazoezini pia Morogoro ila mazoezi ni tofauti na mechi kwa kiwango kikubwa ni usajili mzuri kwani wengi ni vijana wana hari na kupenda kujifunza lakini hata mtazamo wao ni wa kiushindani uku umri wao wa wastani ukiwa ni sababu tosha ya kuwaongezea shauku ya kushindana namzugumzia,Balama Mapinduzi,Ally Mtoni,Kalengo,Mustafa,Sibomana,Balinya,Shikalo,Lamine na Muharami ukiangalia ni vijana ambao wana vipaji na bado wanafundishika jambo linalotoa nafasi kwa benchi la ufundi kuweza kuwatumia kwa kadri ya mipango yao katika hili natoa hongera zangu kwani wamesajili vizuri..Achilia mbali vijana wengine amba jana hawakupata nafasi ya kucheza kama ally alli,Makame,na metacha ambao pia wana uwezo mzuri pia..

  HALI YA MCHEZO WA JANA.
  Jana ndio siku ambayo Yanga SC ilipata kipimo sahihi kwani mechi nyingi za awali huko Morogoro zilikuwa ni za chini kama siyo kawaida hivyo hali halisi ya ushindani haikuwa nzuri. Kwanza nimeona mabadiliko ya kimfumo kwani tumezoea kuona yanga ikicheza mfumo wa 4-2-3-1 tangu mwalimu Zahera ajiunga na timu na kuna wakati alikuwa akitumia mfumo wa 4-4-2 pia jambo ambalo lilifanya yanga kutumia mda mwingi mshambuliaji  mmoja na nguvu kubwa ilitumiaka kwenye winga..Lakini katika mechi ya jana nimeona mabadiliko ya mfumo na kuwa 3-5-2 ambapo upande wa ulinzi kulikuwa na Lamine kama beki wa kati,kulia Mustafa na kushoto Ally Mtoni.Sehemu ya kiungo kulikuwa na viungo 5 sehemu ya kati Papyy Kabamba,akiwa sambamba na Banka na Balama huku pembeni kushoto Muharani na kulia Sibomana huku mbele kukiwa na washambuliaji wawili Sadney na Balinya.
  Kiuchezaji ni mfumo mzuri ambao unaiwezesha timu kumiliki mpira mda mwingi na kushambulia kupitia pembeni uku ikimudu vema kufanya mashambulizi ya kushitukiza kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wachezaji kuanzia endeo la kati kwenda mbele kwani kunakuwa na wachezaji 6 hadi 7  kitu ambacho kama ukiwa na wachezaji shapu na wenye mbio ni rahisi kupata mabao lakini pia ni mfumo ambao kama ukitumika vizuri unafanya timu pinzani kushindwa kupitia kati na kuwalazimu kupitia pembeni muda mwingi wa mchezo.
  Katika mfumo huu mpya ambao jana ulitumia pia niligundua mapungufu yafuatayo:.
  1_ Yanga walikuwa wazuri kushambulia kutoke nyuma ila walikosa uwiano pale walipopoteza mpira na kuwa na idadi ndogo ya walinzi na endapo Kariobang wangekuwa makini wangepata mabao mengi kwani viungo walichelewa kurudi kuzuia na kutoa nafasi kubwa kufanya walinzi wake 3 kucheza kwenye umbali mkubwa ndio mana hata goli la Sharks lilipitia kati kwani Yanga walikosa uwiano katika eneo hilo.
  2_ Bado maelewano ya Kabamba,Banka na Balama hayapo sawa muda mwingi Kabamba anakimbia maeneo mengi na kutozingatia eneo la kiungo cha nyuma jambo lilipelekea muda mwingi Balama kuingia ndani na kusaidia kukaba na kupunguza kasi ya kuisukuma timu mbele pamoja na Banka na kufanya Balinya kushuka chini na Sadney kusogea pembeni kutafuta uwezekano wa kupata mipira mda mwingi hivyo kwa tabia ya kabamba kupangwa kama kiungo mkabaji inaweza kuwagharimu yanga endapo itakutana na timu yenge winga zenye kasi..
  3_ Kukosekana kwa mchezaji ambaye anauwezo wa kupiga pasi ndefu ili kutumia mashambulizi ya kushitukiza kwani Sadney ni mpambanaji na anauwezo wa kuwalazimisha walinzi wa timu pinzani kufanya makosa lakini pia sadney asitumike kama mshambuliaji wa mwisho badala yake awe mshambuliaji wa pili ili aifanye kazi ya kukimbizana na mabeki..
  Hayo ni baadhi ya mapungufu ingawa kwa upande wa staminia na pumzi timu ipo vizuri sana nimeona wachezaji wakiutaka mpira mda wote tofauti na msimu uliopita ambapo wachezaji walikuwa wanatembea uwanjani na kukosa hamu ya kuucheza mpira.
  4_ Bado muunganiko wa kitimu haujakaa sawa sehemu kubwa ni uwezo wa mchezaji mmojammoja hivyo kuna hitajika jitihada za makusudi kulinganisha na muda uliobaki ili kupata muunganiko wa timu ili sasa timu itembee kwenye mdundo mmoja na hii imechangiwa na kukosa mechi ngumu za kiushindani kwa mda wote wa kambi..lakini pia kwa kikosi kilichopo ni vema wakatumia zaidi mfumo wa 4-3-3 kwani wachezaji wenye kasi,ubunifuni,unyumbulifu na maarifa wanao jambo ambalo litawapa faida kubwa na kupata matokeo..
  Mwisho, nitoe ushauri kwa uongozi wa timu kuwa huu sio wakati wa kushangilia mafanikio ya jana ni wakati wa kufanya kazi ule umati wa jana unatakiwa kulindwa na kuongezwa na si jambo dogo ni jitihada zifanyike na kuwa wamoja ili mafanikio yaliyoanza kuonekena yazidi kunawiri vinginevyo itakua ni kama ndoto za mchana ambazo uwa tamu lakini fupi,lakini lazima wajihadhari na migogoro ya kutengenezwa kwani migogoro hiyo huwa na faida kwa wanaoianzisha na uvuruga sana mshikamano ndani ya timu lazima kazi ifanyike na kuleta umoja na kuendeleza mazuri ambayo yameanza kuonekana.
  Pia ni vema kuhakikisha kuwa changamoto mbalimbali za wachezaji na timu kwa ujumla zinatatuliwa na kama ambavyo uongozi uliamua kuacha jukumu la usajili kwa mwalimu basi waendelee kumuamini ili afanye kazi kitaalamu na kama kuhukumiwa iwe baada ya kumpa yale aliyoyataka ili kufanikisha ushindi..
  Kwa kumalizia nawatakiwa maandalizi mema ya mchezo wa hatua ya awali dhidi ya Township Rollers utakaofanyika mwishoni mwa wiki hii. Asanteni kwa jana nimewakubali saluti kwenu hata sisi Stand United tutajifunza kwa yale ya wiki nzima ya Mwananchi.

  (Dominick Salamba ni mchambuzi wa soka na anapatikana kupitia Instagram akaunti yake kupitia@dominicksalamba na anapatikana pia kwa namba +255 713 942 770)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAOMBA NIONGEE NANYI BAADA YA WIKI YA MWANANCHI KUPITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top