• HABARI MPYA

    Thursday, March 01, 2018

    BILA BIMA MCHEZAJI YEYOTE HAGUSI UWANJANI LIGI KUU MSIMU UJAO

    Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
    KUANZIA msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara hakuna mchezaji ataruhidiwa kucheza bila kuwa na Bima.
    Hayo yamesemwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia leo wakati wa ufunguzi wa semina ya utawala bora kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza iliyofanyika katika hoteli ya Rombo Green View, Shekilango mjini Dar es Salaam ambayo ilihusisha klabu zote, zikiwemo kongwe za Simba na Yanga.
    Mwenyekiti wa ISDI, Dk. Tumaini Katuzi (kushoto) akieleza jambo katika semina hiyo. Kulia ni Rais wa TFF, Wallace Karia 
    Semina hiyo iliandaliwa na Kampuni ya Maendeleo na Utafiti wa Michezo (ISDI) kwa kushirikiana na Alliance Life Asuarance na TFF kwa lengo la kutoa elimu kwa viongozi wa klabu kujua jinsi ya utawala, kujiongoza na kutafuta wadhamini.
    Mwenyekiti wa kampuni hiyo Tumain Katunzi amesema wameamua kufanya semina hiyo kla viongozi wa klabu zinazoshiriki ligi zilizo chini ya shirikisho la soka nchini, baada ya kufanya utafiti na kubaini baadhi ya changamoto ambazo zimekua kikwazo katika maendeleo.
    Wakati huo huo Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF Wallece Karia akakazia kauli yake aliyoitoa awali kwa kuwataka wadau wa soka nchini kupitia viongozi wa klabu waliohudhuria semina hiyo, kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa weledi na wasitarajie kama kutakua na urafiki dhidi yake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BILA BIMA MCHEZAJI YEYOTE HAGUSI UWANJANI LIGI KUU MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top