• HABARI MPYA

  Friday, November 10, 2017

  UEFA YAMFUNGIA MIEZI SABA EVRA NA MARSEILLE YAMVUNJIA MKATABA

  KLABU ya Marseille ya Ufaransa imemvunjia mkataba beki wake, Patrice Evra kufuatia mchezaji huyo kufungiwa miezi saba na Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA). 
  Beki huyo wa zamani wa Manchester United alimpiga teke shabiki wa klabu hiyo kabla ya mechi ya Europa League dhidi ya Vitoria wiki iliyopita.
  Mara tu baada ya tukio hilo, klabu hiyo ya Ufaransa ilimsimamisha mchezaji huyo ili uchunguzi ufanyike na sasa wamethibitisha hatua hiyo baada ya kujiridhisha mchezaji huyo alifanya kitendo cha aibu.

  Patrice Evra akimpiga teke shabiki wa Marseille ambalo linamponza kufukuzwa katika klabu hiyo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Picha za tukio hilo zinakumbushia tukio la gwiji mwingine wa Ufaransa, Eric Cantona kumpiga teke la 'kung-fu' shabiki wa Crystal Palace wakati akiichezwa United mwaka 1995.
  Marseille, ambayo ilitozwa faini ya Pauni 22,000 kwa mashabiki wake kuvamia uwanjani, awali ililaani kitendo hicho.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UEFA YAMFUNGIA MIEZI SABA EVRA NA MARSEILLE YAMVUNJIA MKATABA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top