• HABARI MPYA

    Wednesday, November 22, 2017

    ABDI BANDA AIWEKA KILELENI BAROKA FC LIGI KUU AFRIKA KUSINI

    Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
    BEKI Abdi Banda jana ameiongoza timu yake, Baroka FC kutoa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Cape Town City Uwanja wa Cape Town katika mchezo wa Ligi Kuu ya ABSA nchini Afrika Kusini.
    Kwa sare hiyo ya ugenini, Baroka FC inaendelea kuongoza Ligi Kuu ya Absa Afrika Kusini baada ya kujikusanyia pointi 18 kwenye michezo 11.
    Banda alicheza kwa dakika zote 90 na pamoja na safu ya ulinzi ya Baroka kuruhusu bao, moja lakini hakuna shaka kijana alifanya kazi nzuri.
    Abdi Banda jana ameiongoza Baroka FC kutoa sare ya 1-1 na Cape Town City 

    Robin Ngalande alianza kuifungia Baroka dakika ya 55 kabla ya Craig Martin kuwasawazishia wenyeji dakika ya 69.
    Baroka sasa inazizidi kwa pointi mbili zote, Golden Arrows na Cape Town City FC zenye pointi 16 kila moja baada ya kucheza mechi 11 pia.
    Mabingwa watetezi, Bidvest Wits waliojaribu bila mafanikio mara mbili kumsajili kiungo wa Simba, Jonas Mkude wanashika nafasi ya pili kutoka mkiani kwa pointi zake nane za mechi 10, wakati Platinum Stars ndio inaburuza mkia katika ligi ya timu 16 ikiwa imecheza mechi 10 na kuvuna pointi saba.   
    Mabingwa wa kihistoria wa taji la PSL, mara saba, Mamelodi Sundowns wanashika nafasi ya nne kwa pointi zao 15, lakini wamecheza mechi nane tu.
    Jonas Mkude alipokuwa Bidvest Wits kwa majaribio. Timu iliyomtaka imeuanza msimu huu vibaya

    Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini inaendelea leo kwa michezo minne, timu ya zamani ya Mrisho Ngassa, Free State Stars itaikaribisha Chippa United Uwanja wa Goble Park, Platinum Stars watakuwa wenyeji wa Bloemfontein Celtic Uwanja wa Royal Bafokeng, AmaZulu FC wataikaribisha Kaizer Chiefs Uwanja wa King Zwelithini na Polokwane City watakuwa wenyeji wa Maritzburg United Uwanja wa Old Peter Mokaba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ABDI BANDA AIWEKA KILELENI BAROKA FC LIGI KUU AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top