• HABARI MPYA

    Friday, November 24, 2017

    UTAWALA WA MAKOCHA WA AFRIKA KOMBE LA SHIRIKISHO KUENDELEA

    UTAWALA wa makocha wa Kiafrika dhidi ya wa Ulaya unatarajiwa kuendelea kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika kesho.
    Hiyo ni katika mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho, SuperSport United wakiikaribisha TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia (DRC) Uwanja wa Lucas Masterpieces Moripe mjini Pretoria, Afrika Kusini.
    Mchezo wa kwanza Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi, Novemba 19, TP Mazembe walishinda 2-1 na leo watahitaji sare ugenini ili kushinda taji la 11 la CAF, huku SuperSport wakiwania taji la kwanza.
    Kocha wa SuperSports United ya Afrika Kusini, Eric Tinkler anatakiwa kupindua matokeo ya kipigo cha 2-1 kubeba Kombe la Shirikisho mbele ya Pamphile Mihayo wa TP Mazembe

    SuperSport inafundishwa na kiungo wa zamani wa Afrika Kusini, Eric Tinkler na Mazembe inafundishwa na mchezaji wake wa zamani, Mkongo, Pamphile Mihayo.
    Fainali 13 za michuano hiyo inayofananishwa na Europa League ya UEFA zimekwishafanyika na klabu tisa za makocha Waafrika zimeshinda taji hilo.
    Mkongwe wa Tunisia, Faouzi Benzarti amebeba taji hilo mara mbili akiwa na Etoile Sahel, mwaka 2006 na 2015.
    Ni kati ya makocha watatu walioshinda Kombe la Shirikisho na wakashinda pia Ligi ya Mabingwa, akipata mafanikio akiwa na klabu ya Esperance.
    Makocha wengine wawili wazawa waliotwaa mataji yote ya klabu barani AfrikaThe ni Mghana Cecil Jones Attuquayefio, aliyefariki dunia mwaka 2015 na Mmorocco Hussein Amotta. 
    Attuquayefio alishinda mataji yote akiwa na vigogo wa Accra, Hearts of Oak wakati Amotta alibeba Kombe la Shirikisho akiwa na FUS Rabat na Ligi ya Mabingwa mwaka huu akiwa na Wydad Casablanca. 

    MAKOCHA WALIOTWAA KOMBE LA SHIRIKISHO
    2004: Cecil Jones Attuquayefio (Hearts of Oak/Ghana)
    2005: Mohamed Fakhir (FAR Rabat/Morocco)
    2006: Faouzi Benzarti (Etoile Sahel/Tunisia)
    2007: Michel Decastel, SUI (CS Sfaxien/Tunisia)
    2008: Ghazi Ghrairi (CS Sfaxien/Tunisia)
    2009: Djibril Drame (Stade Malien/Mali)
    2010: Hussein Amotta (FUS Rabat/Morocco)
    2011: Rachid Taoussi (MAS Fes/Morocco)
    2012: Joseph Omog, CMR/Cyril Ndonga (AC Leopards/Kongo) 
    2013: Ruud Krol, Mholanzi (CS Sfaxien/Tunisia)
    2014: Juan Carlos Garrido, Hispania (Al Ahly/Misri)
    2015: Faouzi Benzarti (Etoile Sahel/Tunisia)
    2016: Hubert Velud, FRA (TP Mazembe/Kongo)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UTAWALA WA MAKOCHA WA AFRIKA KOMBE LA SHIRIKISHO KUENDELEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top