• HABARI MPYA

  Saturday, May 20, 2017

  ZIDANE ATEUA 25 KUFUATA 'NDOO' YA LA LIGA KESHO ROSALEDA

  KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane ameteua wachezaji 25 kwa ajili ya mchezo wa ugenini wa La Liga kesho dhidi ya Malaga.
  Real Madrid watasafiri hadi La Rosaleda kwa mchezo wa mwisho wa LaLiga wakihitaji sare tu kujihakikishia ubingwa.
  Timu ya Zidane kwa sasa ina pointi 90, ikifuatiwa na wapinzanji wao wakubwa, Barcelona wenye pointi 87 baada ya kila timu kucheza mechi 37.
  Barcelona wenye wastani mzuri wa mabao kuliko Real wanaweza wakachukua taji la La Liga wakishinda kesho dhidi ya Eibar kama Madrid watafungwa na Malaga.
  Zinedine Zidane ameteua wachezaji 25 kwa ajili ya mchezo wa ugenini wa La Liga kesho dhidi ya Malaga

  Na kwa kuhakikisha wanamaliza ligi vizuri na kutwaa taji, Zidane ameteua cha nguvu kwa ajili ya mchezo huo.   
  Makipa; Navas, Casilla na Yanez.
  Mabeki: Carvajal, Pepe, Ramos, Varane, Nacho, Marcelo, Coentrão na Danilo.
  Viungo: Kroos, James, Casemiro, Kovacic, Modric, Asensio, Isco na Enzo.
  Washambuliaji: Cristiano Ronaldo, Benzema, Bale, Lucas Vázquez, Mariano na Morata.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZIDANE ATEUA 25 KUFUATA 'NDOO' YA LA LIGA KESHO ROSALEDA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top