• HABARI MPYA

    Sunday, May 21, 2017

    SAMATTA AENDELEA KUNG’ARA GENK

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana amecheza vizuri kwa dakika zote 90 timu yake, KRC Genk ikilazimisha sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Lokeren Uwanja wa Daknam mjini Lokeren, Ubelgiji kwenye mchezo wa Kundi B kuwania tiketi ya kucheza michuano ya UEFA Europa League mwakani.
    KRC Genk walitangulia kwa bao la penalti la kiungo mkongwe wa umri wa miaka 33, Mbelgiji Koen Persoons aliyejifunga dakika ya nne, kabla ya mshambuliaji mwenye umri wa miaka 31, Mbelgiji pia Tom De Sutter kuisawazishia Lokeren dakika ya 57.
    Pamoja na sare hiyo, Genk inaendelea kuongoza Kundi B katika mchuano wa kuwania tiketi ya Europa League mwakani kwa kufikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi tisa na Samatta jana ameichezea Genk mechi ya 58 tangu ajiunge nayo Januari mwaka jana kutoka TP Mazembe ya DRC akiwa amefunga mabao 19.
    Kati ya mechi hizo 58, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 40 msimu huu na kati ya hiyo, ni michezo 36 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 26 msimu huu.
    Mechi 21 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 13 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, tano msimu uliopita na sita msimu huu na katika mabao hayo 19, 14 amefunga msimu huu na tano msimu uliopita.
    Kikosi cha Lokeren kilikuwa: Verhulst, Skulason, Single, De Sutter/Enoh dk65, Terki, Huppert/Rocketman Stra dk76, Ticinovic, Rassoul/Martin dk63, Miric, Knight na Monsecour.
    KRC Genk : Ryan, Nastic, Wouters, Seigers, Castagne, Berge, Kumordzi/Heynen dk61, Sabak/Writers dk76, Naranjo, Buffalo/Vermijl dk45 na Samatta.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA AENDELEA KUNG’ARA GENK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top