• HABARI MPYA

  Monday, May 22, 2017

  NI MALI NA GUINEA LIBREVILLE, GHANA NA NIGER PORT GENTIL

  TIMU ya Mali itamenyana na Guinea katika Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka Jumatano mjini Libreville, Gabon.
  Hiyo inafuatia ushidi wa mabao 6-1 dhidi ya Angola katika mchezo wa mwisho wa Kundi B Uwanja wa l’Amitie mjini Libreville.
  Niger itamenyana na Ghana mjini Port Gentil katika Nusu Fainali nyingine ya michuano hiyo Jumatano pia. Ghana na Guinea zimefuzu kutoka Kundi A lililokuwa pia na timu za wenyeji, Gabon na Cameroon ambazo zimetolewa, wakati Mali na Niger zimetokea Kundi B lililokuwa pia na timu za Tanzania na Angola ambazo zimeaga mashindano hayo.
  Niger wakishangilia baada ya ushindi wao dhidi ya Tanzania jana

  Tanzania imetolewa katika michuano hiyo baada ya kufungwa 1-0 na Niger katika mchezo wa mwisho wa Kundi B usiku huu Uwanja wa Port Gentil mjini Gentil jana.
  Matokeo hayo yanazifanya Niger na Tanzania zifungane pointi na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa, hivyo mshindi katika mechi baina yao anafuzu Kombe la Dunia Oktoba mwaka huu India na pia kwenda Nusu Fainali ya michuano hiyo.
  Niger anaungana na Mali iliyoongoza kundi kwa pointi zake saba, baada ya ushindi wa mechi mbili na sare moja, wakati Tanzania na Angola zote zinatolewa.
  Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Daniel Laryea wa Ghana, aliyesaidiwa na 
  Seydou Tiama wa Burkina Faso na Attia Amsaad wa Libya, Niger walipata bao lao kipindi cha kwanza, mfungaji Ibrahim Boubacar Marou dakika ya 41 baada ya shambulizi zuri lililowachanganya walinzi wa Serengeti Boys.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI MALI NA GUINEA LIBREVILLE, GHANA NA NIGER PORT GENTIL Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top