• HABARI MPYA

  Sunday, May 21, 2017

  MJOMBA AVAMIA ULINGONI KUMPIGA MPINZANI WA DIRRELL

  MJOMBA wa bingwa wa dunia wa uzito wa Super-Middle, Andre Dirrell usiku wa kuamkia leo amemshambulia kwa makonde ulingoni mpinzani wa mpwa wake, Jose Uzcategui kwa kuendelea kumpiga nduguye baada ya kengele katika pambano lao.
  Katika pambano hilo lililofanyika ukumbi wa MGM National Harbor mjini Maryland, kocha Leon Lawson alipanda ulingoni kumshambulia Uzcategui baada ya pambano hilo la mkanda wa IBF.
  Mvenezuela huyo alitandikwa ngumo ya kushoto na Lawson, ikifuatiwa na ya kulia kabla ya wawili hao kutenganishwa.
  Mshauri wa Uzcategui, Sean Gibbons akawaambia Waandishi wa Habari atafungua kesi kwa tukio hilo.
  Mpinzani wa Andre Dirrell, Jose Uzcategui akirushiwa konde na mjomba na wa mpinzani wake baada ya pambano jana  
  When you check up on last night's US fights and find out Dirrell won by DQ for being KO'd after bell and his uncle wanted some revenge!
  Uzcategui alipelekwa hospitali ya MedSTAR Washington mjini Washington DC kwa matibabu kabla ya kuruhusiwa baadaye kwa mujibu wa ESPN.  
  Polisi wanamshikilia Lawson kwa maswali zaidi juu ya tukio hilo. Dirrell alishinda pambano hilo usiku wa jana baada ya Uzcategui kurudia mara mbili kumshambulia mwenzake baada ya kengele kupigwa.
  Alikwenda chini na kusema hawezi kuendelea kufuatia kupigwa baada ya kengele na mpinzani wake akaondolewa mchezoni.  
  Refa Bill Clancy alisema mapema tu alimuonya Mvenezuela huyo juu ya kurusha makonde baada ya kengele na imemgharimu kupoteza pambano ambako alikuwa anaelekea kushinda.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MJOMBA AVAMIA ULINGONI KUMPIGA MPINZANI WA DIRRELL Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top