• HABARI MPYA

  Thursday, October 20, 2016

  MPAMBANO WA LEYLA RASHID NA ISHA MASHAUZI JUMAMOSI HII …ni vita ya “Sura Surambi” na “Nina Moyo Sio Jiwe”

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NI vita ya “Sura Surambi” na “Nina Moyo Sio Jiwe”.  Ndiyo unavyoweza kusema kuelekea mpambano wa waimbaji nyota wa taarab malkia Leyla Rashid na Isha Mashauzi.
  Onyesho hilo linasosubiriwa kwa hamu kubwa litafanyika Jumamosi ya tarehe 22 mwezi huu ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Saalam.
  Bendi mbili kubwa za taarab, Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic ndiyo zitakazosindikiza mpambano wa mahasimu hao wawili.
  “Sura Surambi” ni moja ya nyimbo ambazo piga ua lazima iwe kweye ratiba ya Isha Mashauzi wakati iwe isiwe Leyla naye lazima aidumbukize ngoma yake ya “Nina Moyo Sio Jiwe” katika orodha ya nyimbo atakazotumbuiza.
  Tangu onyesho hilo litangazwe, waimbaji hao wameingia kwenye vita vikubwa vya maneno ambapo kila mmoja amejinasibu kuibuka na ushindi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MPAMBANO WA LEYLA RASHID NA ISHA MASHAUZI JUMAMOSI HII …ni vita ya “Sura Surambi” na “Nina Moyo Sio Jiwe” Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top