• HABARI MPYA

  Friday, June 03, 2016

  SHERMAN 'ATIMULIWA' MPUMALANGA, KISA...

  KLABU ya Mpumalanga Black Aces imevunja Mkataba na mshambuliaji Mliberia, Kpah Sherman (pichani kulia) baada ya msimu mmoja tu tangu imsajili kutoka Yanga SC ya Tanzania.
  Hiyo inafuatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kucheza mechi tano tu, tena mbili ndiyo akianza na tatu akitokea benchi bila ya kufunga hata bao moja.
  Wakamtoa kwa mkopo Santos ya Cape Town, ambako huko pamoja na kucheza Ligi Daraja la Kwanza, alifunga bao moja tu katika mechi nne alizoanza.
  Kabla ya mwanzo wa msimu, kocha Muhsin Ertugral alibashiri mzaliwa huyo wa Monrovia atarudi kwa kishindo Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini, lakini baadaye akasema ni mmoja wa waliyeigharimu timu katika msimu huu.
  Kabla ya Yanga ambako alicheza kwa msimu mmoja pia, Sherman awali alicheza Sweden na Cyprus ya Kaskazini na pia amewahi kuchezea timu yake ya taifa.
  Sherman amekuwa na mwanzo mzuri kila klabu anayoenda na kuwavutia makocha na mashabiki, lakini baadaye hutekwa na starehe kiasi cha kupoteza mwelekeo wa kisoka na kufikia kuwa mzigo katika klabu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SHERMAN 'ATIMULIWA' MPUMALANGA, KISA... Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top