• HABARI MPYA

    Friday, June 03, 2016

    MASHAUZI, SNURA, ROMA MKATOLIKI NA WAZEE WA SINGELI KUISHIKA DAR LIVE JUMAMOSI HII

    JUMAMOSI hii ya Juni 4 mbona  ‘kitanuka’ Dar Live! Ni usiku wa nani mkali kutoka kwa mastaa wa taarab, bongo fleva na singeli.
    Ni onyesho kubwa la na mwisho kabla kuelekea mapumziko ya mwezi mtufu wa Ramadhan ambapo Isha Mashauzi akiwa na kundi zima la Mashauzi Classic ataumana jukwaa na Snura, Roma Mkatoliki, Sholo Mwamba na Man Fongo.
    Msemaji wa ukumbi wa Dar Live, Juma Mbizo amesema onyesho hilo la kipekee limezingatia muziki wa kila njanja ili kuleta ladha isiyochuja mwanzo hadi mwisho wa show.
    Mbizo amesema kupitia onyesho hilo mashabiki watajionea wenyewe ni mzuiki upi wenye nguvu zaidi kati ya taarab, bongo fleva, singeli na hata rumba kutokana na ukweli kuwa Isha Mashauzi mbali na taarab lakini pia ana ngoma zake kali za muziki wa rumba.
    Naye Isha Mashauzi amesema atalitendea haki onyesho hilo hasa kutokana na ukweli kuwa hajapanda jukwaa la Dar Live kwa takriban miaka miwili na hivyo hiyo ni nafasi pekee ya kutaka kiu ya mashabiki wake watakaofika kwenye ukumbi huo mkubwa zaidi wa burudani ulioko maeneo ya Mbagala jijini Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MASHAUZI, SNURA, ROMA MKATOLIKI NA WAZEE WA SINGELI KUISHIKA DAR LIVE JUMAMOSI HII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top