• HABARI MPYA

  Thursday, June 09, 2016

  HODGSON AWAFUNIKA MAKOCHA WOTE EURO 2016 KWA KUVUTA 'MKWANJA MNENE'

  KOCHA wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson ndiye anayelipwa zaidi ya makocha wote wa Euro 2016, akiwa anaingiza kiasi cha Pauni Milioni 3.5 kwa mwaka akimpiku Antonio Conte wa Italia, anayefuatia kwa kulipwa Pauni Milioni 3.15 na Fatih Terim wa Uturuki anashika nafasi ya tatu kwa kulipwa Pauni Milioni 2.7.
  Makocha wanane kati ya 24 wanaingiza Pauni Milioni kila mmoja kwa mwaka - lakini mmoja tu, Leonid Slutsky haingizi kitu. Slutsky pia ni kocha wa CSKA Moscow na amechukua majukumu ya timu yake ya taifa kuokoa jahazi baada ya Fabio Capello kuondoka.
  Wakati Slutsky anapewa timu ya taifa majira ya joto yaliyopita, Waziri wa MIchezo Vitaly Mutko alithibitisha: "Hatakuwa na mshahara, isipokuwa posho kulingana na matokeo,".
  Kocha wa England, Roy Hodgson ndiye anaongoza kulipwa kati ya makocha wote wa Euro 2016 akiwa anapata Pauni Milioni 3.5 kwa mwaka  PICHA ZAIDI GONGA HAPA  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HODGSON AWAFUNIKA MAKOCHA WOTE EURO 2016 KWA KUVUTA 'MKWANJA MNENE' Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top