• HABARI MPYA

    Friday, June 03, 2016

    CHEKA ULINGONI KESHO TAIFA, KUZIPIGA NA MBABE WA MALAWI

    Na Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM
    BONDIA nyota wa ngumi za kulipwa nchini, Cosmass Cheka (pichani kulia) kesho anapanda ulingoni Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam kupambana na bondia wa Malawi, Chrispin Moliyati katika pambano la kuwania ubingwa wa Universal Boxing Union (UBO) wa uzito wa Super Feather.
    Pambano hilo la raundi 12 limeandaliwa na Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Advanced Security, Juma Ndambile kwa lengo la kuendeleza mchezo wa ngumi za kulipwa nchini.
    Ndambile  ambaye ni meneja wa Cheka alisema kuwa ameaua kumtuafutia mpinzani wa nje bondia wake kwa lengo la kumpandisha kiwango ili aweze kucheza mapambano makubwa duniani.
    Alisema kuwa ameamua kuondokana na kuwaandalia mabondia wake mapambano dhidi ya mabondia wa hapa hapa kwani hawapati uzoefu wa kimataifa.
    Kwa upande wake, Cheka alisema kuwa amejiandaa vyema kwa  pambano hilo na anataka kuonyesh ubora wake katika mchezo wa ngumi za kulipwa.
    Cheka alisema kuwa anatarajia kushinda katika pambano hilo ili kuendeleza rekodi yake katika  ngumi za kulipwa.
    “Moliyati ni bondia mzuri na najua atanipa upinzani mkali, lakini sitakubali kupoteza katika ardhi ya Tanzania, nimejiandaa vizuri kwa ajili ya pambano hilo,” alisema.
    Mbali ya mapambano hayo, leo pia kutakuwa na ‘mawe’ ya aina yake katika mapambano ya utangulizi.
    Bondia nyota, Japhet Kaseba atawania ubingwa wa Taifa wa TPBC Limited dhidi ya bondia nyota kutoka Zanzibar, Amour Mzungu katika pambano la uzito wa juu,  Pia Alphonce Mchumiatumbo atazipiga na bondia Mussa Ajibu kutoka Malawi katika pambano la uzito wa juu kabla ya Ashraf Suleiman kuonyeshana kazi na Aliki Gogodo wa Malawi katika pambano la uzito wa juu pia.
    Pambano lingine la ubingwa litakuwa kati ya bondia Shabani Kaoneka dhidi ya Zumba Kukwe la uzito wa middle raundi 10 ambapo Yonas Segu atazichapa na bondia wa Malawi, Wilson Masamba katika pambano la uzito wa Light-Welter la raundi nane.
    Mabondia wa kike, Lulu Kayage atazichapa na Enelesi Nkwanthi katika pambano la uzito wa bantam la raundi sita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHEKA ULINGONI KESHO TAIFA, KUZIPIGA NA MBABE WA MALAWI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top