• HABARI MPYA

  Wednesday, October 02, 2019

  TANZANIA BARA YAITOA SUDAN CECAFA CHALLENGE U20, KUKUTANA NA KENYA FAINALI JUMAMOSI

  Na Mwandishi Wetu, GULU 
  TANZANIA Bara imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, CECAFA Challenge U20 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Sudan jioni ya leo Uwanja wa Guru nchini Uganda.
  Na sasa Tanzania itakutana na Kenya katika fainali Jumamosi Uwanja wa Kituo cha Ufundi cha Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), wakati Sudan itamenyana na Eritrea katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.
  Katika mchezo wa leo, mabao ya Tanzania Bara iliyo chini ya kocha wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila yamefungwa na Israel Patrick Mwenda dakika ya 36 na Kelvin Pius John dakika ya 45, wakati la Sudan limefungwa na Mohamed Abbas Namir dakika ya 56.

  Na bao pekee la Kenya leo hii alijifunga mchezaji wa Eritrea, Yosief Mebrahtu dakika ya 84. Ikumbukwe Kenya na Tanzania zimetoka kundi moja, B na mechi baina yao ilimalizika kwa sare ya 2-2.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA BARA YAITOA SUDAN CECAFA CHALLENGE U20, KUKUTANA NA KENYA FAINALI JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top