• HABARI MPYA

  Sunday, August 04, 2019

  MAN CITY WAIPIGA LIVERPOOL KWA PENALTI NA KUBEBA NGAO YA JAMII

  Sergio Aguero (katikati kushoto) na David Silva (katikati kulia)  wakiinua Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Liverpool kufuatia sare ya 1-1 Uwanja wa Wembley mjini London leo. Raheem Sterling alianza kuifungia Manchester City dakika ya 23 akimalizia pasi ya Silva, kabla ya Joel Matip kuisawazishia Liverpool dakika ya 77 akimalizia pasi ya beki Virgil van Dijk.
  Kwenye mikwaju ya penalti, Xherdan Shaqiri, Adam Lallana, Alex Oxlade-Chamberlain na Mohamed Salah waliifungia Liverpool, wakati Georginio Wijnaldum alikosa na Ilkay Gundogan, Bernardo Silva, Phil Foden,Oleksandr Zinchenko na Gabriel Jesus waliifungia Man City 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY WAIPIGA LIVERPOOL KWA PENALTI NA KUBEBA NGAO YA JAMII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top