• HABARI MPYA

  Thursday, December 13, 2018

  NINI TENA 'CHA UKOROFI' POGBA ANAMLETEA REFA HAPA!

  Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba akimkoromea refa Mbulgaria, Georgi Kabakov baada ya kutofurahishwa na maamuzi yake wakati wa mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya wenyeji, Valencia usiku wa jana Uwanja wa Mestalla. 
  Man United ilifungwa 2-1, mabao ya wenyeji yakifungwa na Carlos Soler dakika ya 17 na Phil Jones aliyejifunga dakika ya 47 na lao akifunga Marcus Rashford dakika ya 87 baada ya kutokea benchi kuchukua nafasi ya Fred dakika ya 57.
  Manchester United imemaliza na pointi 10 nyuma ya Juventus iliyomaliza na pointi 12 na zote zinasonga mbele hatua ya 16 Bora zikizipiku Valencia iliyomaliza na pointi nane na Young Boys pointi nne 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NINI TENA 'CHA UKOROFI' POGBA ANAMLETEA REFA HAPA! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top