• HABARI MPYA

    Wednesday, December 19, 2018

    DROO YA UPANGAJI WA MAKUNDI NA RATIBA YA MICHUANO YA AFCON U17 MWAKA 2019 KUFANYIKA KESHO MLIMANI CITY

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    UPANGAJI wa ratiba wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 (AFCON U17) zitakazofanyika Mei mwakani 2019 nchini, utafanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mlimani City mjini Dar es salaam.
    Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Mario Ndimbo amesema kwamba maandalizi yote yamekamilika kuelekea zoezi hilo.
    Ndimbo amesema kwamba Rais wa TFF, Wallace Karia tayari amepokea ugeni kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambao upo nchini kwa upangaji wa ratiba.

    Serengeti Boys watapangiwa wapinzani gani kesho AFCON U17 mwaka 2019?

    Amesema ujumbe huo wa CAF ukiwa hapa nchini umetembelea kukagua uboreshaji wa miundo mbinu ya viwanja unaoendelea na Karia amesema baada ya kutazama maendeleo ya Viwanja watashauri zaidi kulingana na walivyoona maendeleo hayo.
    Ndimbo amesema mbali na Viwanja ujumbe huo wa CAF umetembelea Hoteli na Hospitali na kesho utahudhuria upangaji wa ratiba ya fainali hizo utakaofanyika kuanzia saa 12:00 jioni na Dunia itapata kushuhudia upangaji huo moja kwa moja kwenye Televisheni.
    Wajumbe wa CAF waliopo nchini ni Samson Adamu,Yasmin Hossam Eldin El Ehwany,Amri Ali Sadek,Mohamed Bakeer,Fayrouz Mahml,Mohamed Alaa El Shizy,Dina Medat,Moses Magogo anayewakilisha Kamati y Utendaji ya CAF wakati Leodger Tenga Mjumbe wa Kamati ya Utendaji CAF atakua mwenyeji wao.
    Timu zilizofuzu kushiriki AFCON U17 Mei mwakani pamoja na wenyeji, Tanzania nyingine ni Morocco, Senegal, Guinea, Nigeria, Cameroon, Uganda na Angola.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DROO YA UPANGAJI WA MAKUNDI NA RATIBA YA MICHUANO YA AFCON U17 MWAKA 2019 KUFANYIKA KESHO MLIMANI CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top