• HABARI MPYA

  Saturday, December 15, 2018

  MOHAMED ISSA 'BANKA' ARUHUSIWA KUANZA KAZI YANGA SC BAADA YA KUMALIZA ADHABU YA KIFUNGO CHA BANGI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO mpya wa Yanga SC, Mohamed Issa ameruhusiwa kuanza mazoezi wakati akikaribia mwisho wa adhabu yake ya kufungiwa baada ya kubainika kutumia dawa zisizoruhusiwa michezoni aina ya bangi.
  Afisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Mario Ndimbo amesema leo mjini Dar es Salaam kwamba Mohamed Issa, maarufu Banka baada kubainika kutumia dawa hizo alifungiwa kwa kipindi cha miezi 14 kuanzia Disemba 9,2017 na adhabu kumalizika Februari 8,2019.
  Pamoja na kuruhusiwa kuanza mazoezi Mohamed Issa haruhusiwi kucheza mchezo wowote ule zaidi ya kufanya mazoezi.

  Mohamed Issa 'Banka' (kulia) amemaliza adhabu na sasa yuko huru kuanza kazi rasmi Yanga SC
  Mohamed Issa alifungiwa na Kamati ya kuzuia na kupambana na dawa zisizoruhusiwa michezoni ya Kanda ya Tano Africa (RADO).
  Kufunguliwa kwa mchezaji huyo ni habari njema kwa Yanga SC iliyomsajili Julai mwaka huu kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, kwani sasa anakewenda kuongeza nguvu kwenye kikosi cha timu hiyo ya Jangwani, Dar es Salaam. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MOHAMED ISSA 'BANKA' ARUHUSIWA KUANZA KAZI YANGA SC BAADA YA KUMALIZA ADHABU YA KIFUNGO CHA BANGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top