• HABARI MPYA

  Thursday, December 13, 2018

  KAMA HUU NI MPIRA MULLER ASINGETOLEWA KWA KADI NYEKUNDU

  Mshambuliaji wa Bayern Munich, Thomas Muller akimtandika teke Nicolas Tagliafico wa Ajax usiku wa jana Uwanja wa Johan Cruijff Arena mjini Amsterdam katika mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya timu hizo zikitoka sare ya 3-3.
  Refa Mfaransa, Clement Turpin alimtoa Muller kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa rafu hiyo dakika ya 75 na mabao ya Bayern Munich yalifungwa na Robert Lewandowski mawili dakika za 13 na 87 kwa penalti na Kingsley Coman dakika ya 90, wakati ya Ajax yalifungwa na Dusan Tadic mawili dakika za 61 na 82 kwa penalti Nicolas Tagliafico dakika ya 90 na ushei.
  Bayern Munich imemaliza kileleni mwa Kundi E kwa pointi zake 14, ikifuatiwa na Ajax pointi 12 na zote zinazonga mbele hatua ya 16 Bora zikizipiku Benfica iliyomaliza na pointi saba na AEK Athens iliyomaliza bila pointi 
    
    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAMA HUU NI MPIRA MULLER ASINGETOLEWA KWA KADI NYEKUNDU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top