• HABARI MPYA

  Thursday, December 13, 2018

  YOUNG BOYS WAMDUWAZA RONALDO, WAIPIGA JUVENTUS 2-1

  Mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo akisikitika baada ya kupoteza nafasi ya kufunga jana dhidi ya wenyeji, Young Boys Uwanja wa Suisse Wankdorf Bern mjini Bern, Uswisi katika mchezo wa Kundi H Ligi ya Mabingwa Ulaya. 
  Young Boys walishinda 2-1, mabao yao yakifungwa na Guillaume Hoarau yote mawili dakika za 30 kwa penalti na 68, wakati la Juventus lilifungwa na Paulo Dybala dakika ya 80.
  Pamoja na ushindi huo, Young Boys imemaliza nafasi ya mwisho kwenye Kundi H kwa pointi zake nne, nyuma ya Valencia iliyomaliza na pointi nane, Manchester United pointi 10 na Juventus pointi 12, timu mbili za juu zikisonga mbele hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YOUNG BOYS WAMDUWAZA RONALDO, WAIPIGA JUVENTUS 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top