• HABARI MPYA

    Saturday, March 10, 2018

    MAN UNITED KUMKOSA POGBA MECHI NA LIVERPOOL LEO OLD TRAFFORD

    KIUNGO Mfaransa, Paul Pogba yuko hatarini kukosekana kwenye kikosi cha Manchester United kwenye mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Liverpool leo baada ya kuumia mazoezini jana.
    Mchezaji ghali aliyesajiliwa United kw adau la rekodi, Pauni Milioni 89 anapambana na hali yake ili awe fiti kuteremka Uwanja wa Old Trafford leo kucheza.
    Inafahamika Pogba ameumia mguu jana katika mazoezi ya mwisho viwanja vya Carrington na hakumaliza, ingawa bado hajaondolewa rasmi kwenye mchezo wa leo. 
    Man United itapoteza nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England iwapo itafungwa na Liverpool ya kocha Mjerumani, Jurgen Klopp.
    Paul Pogba anaweza kukosekana Manchester United ikimenyana na Liverpool leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

    Pamoja na hayo, Pogba hakuonekana wakati kikosi cha Man United kinaingia kambini jana kwenye hoteli ya Lowry kuelekea mchezo wa leo.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Man United tangu awasili Old Trafford.
    Lakini alitemwa kwenye kikosi kilichomenyana na Huddersfield na Sevilla, na akatolewa katika mchezo dhidi ya Tottenham na Newcastle. Pogba pia alikosekana kwenye mechi ya Kombe la FA Man United wakishinda dhidi ya Huddersfield mwezi uliopita kwa madai alikuwa mgonjwa.
    Baada ya hapo akaanza mechi zote dhidi ya Chelsea na Crystal Palace na kuzima tetesi kwamba ametofautiana na kocha Mreno, Jose Mourinho.
    Eric Bailly pia yuko shakani kuanza leo kwa mara ya kwanza tangu aumie Novemba na kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu, baada ya kutokea benchi mara mbili, lakini Anthony Martial atakuwa nje kwa maumivu ya pua. 
    Anaingia kwenye orodha ya majeruhi wengine akina Ander Herrera, Zlatan Ibrahimovic, Marcos Rojo na Daley Blind ambao wote wanakosekana kwa sasa. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED KUMKOSA POGBA MECHI NA LIVERPOOL LEO OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top