• HABARI MPYA

  Friday, March 02, 2018

  MAJI MAJI NA KAGERA SUGAR 'UJI NA MGONJWA' KESHO KAITABA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MECHI za mzunguko wa 20 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zinatarajiwa kuendelea kesho nyasi za viwanja vinne nchini zikiwaka moto.
  Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Kagera Sugar wakiikaribisha Maji Maji ya Songea kuanzia Saa 10:00 jioni na Njombe Mji watakuwa nyumbani Uwanja wa Saba Saba kucheza na Ruvu Shooting, mchezo utakaochezwa saa 8 mchana.
  Mechi nyingine Tanzania Prisons ya Mbeya watakuwa nyumbani Uwanja wa Sokoine kucheza dhidi ya Mbao FC ya Mwanza saa 10 jioni,Azam FC watakuwa Azam Complex ikiwakaribisha Singida United saa 1 jioni.
  Zote, Njombe Mji, Maji Maji na Kagera Sugar zinafungana kwa pointi 15 kila mmoja mkiani mwa Ligi Kuu, zikizbeba timu nyingine13. 
  Wakati huo huo; Hatua ya Nane Bora Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho na keshokutwa.
  Jumamosi ya kesho; Panama FC vs JKT Queens Uwanja wa Samora mjini Iringa na Jumapili Simba Queens wataikaribisha Evergreen Uwanja wa Karume, Mlandizi na Kigoma Sisters Uwanja wa Mabatini na Baobab na Alliance Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAJI MAJI NA KAGERA SUGAR 'UJI NA MGONJWA' KESHO KAITABA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top