• HABARI MPYA

  Tuesday, November 07, 2017

  TFF YASIMAMISHA MECHI AZAM SPORTS FEDERATION CUP

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limefanyia marekebisho ratiba ya michuano ya Azam Sports Federation Cup.
  Mchezo kati ya Forodhani FC ya Mara na Ambassodor ya Kahama umesimamishwa na mchezo kati ya Bulyanhulu na Area C, sasa utafanyika kesho Jumatano Novemba 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
  Mchezo kati ya Forodhani FC ya Mara na Ambassodor ya Kahama, umesimamishwa kusubiri uamuzi wa Kamati ya Mashindano baada ya Baruti ambayo imelete malalamiko kuhusu nafasi yake.
  Michezo mingine inayochezwa leo Jumanne ni Msange na Mirambo kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi; Pepsi na Kilimanjaro Heroes kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga; Mji Mkuu na Nyundo kwenye Uwanja wa Mpwapwa mkoani Dodoma.
  Eleven Stars itacheza na Ndovu kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera, Changanyikeni itacheza na Reha Uwanja wa Bandari, Dar es Salaam wakati Bodaboda itacheza  na Kitayosce Uwanja wa Nyerere, Mbulu mkoani Manyara.
  Mbali ya mchezo kati ya Bulyanhulu na Area C, mechi nyingine za kesho Jumatano, Novemba 8 zitakuwa ni kati ya Cosmopolitan na Abajalo kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani wakati makumba Rangers watacheza na Green Warriors kwenye Uwanja wa Bandari, Dar es Salaam.
  AFC ya Arusha itaikaribisha Nyanza FC kwenye Uwanja wa Ushirika; Boma Fc na African Sports watacheza kwenye Uwanja wa Ushirika; huku Motochini ikicheza na Ihefu wakati Stand Misuna watacheza na Madini ilihali Burkina FC itaialika Mbinga United kadhalika Mkamba Rangers itacheza na Makambako FC kwenye Uwanja wa Sabasaba.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YASIMAMISHA MECHI AZAM SPORTS FEDERATION CUP Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top