• HABARI MPYA

  Tuesday, November 07, 2017

  AZAM FC ‘YAMTUPIA VIRAGO’ RASTA MGHANA YAHYA MOHAMMED

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam FC imeachana na mshambuliaji wake, Mghana, Yahya Mohammed baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
  Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema kwamba, klabu imeachana na mchezaji huyo rasta baada ya kutoridhishwa na uwajibikaji wake kwenye timu.
  “Yalikuwa makubaliano baina yetu, baada ya sisi kama klabu kutoridhishwa na mchango wake kwetu, hivyo kuanzia sasa yuko huru,”amesema Jaffar.
  Yahya alisajiliwa Azam FC kwa matarajio makubwa Juni mwaka jana kwa dau la dola za Kimarekani, 100,000 zaidi ya Sh. Milioni 220 kutoka Aduana Stars ya kwao.
  Azam FC imeachana na mshambuliaji wake, Mghana, Yahya Mohammed baada ya makubaliano ya pande zote mbili

  Alikuwa miongoni mwa wachezaji watano wa Ghana waliosajiliwa Azam FC wakati huo, wengine ni Daniel Amoah, Enoch Atta Agyei kutoka Medeama SC, Samuel Afful kutoka Sekondi Hasaacas na Yakubu Mohammed kutoka Aduana Stars pia.
  Mwanzoni mwa msimu, Azam FC ilimtema Afful na kumsajili kipa Mghana pia, Razak Abalora kutoka klabu ya Wafa ya kwao. Jaffar amesema baada ya kuondolewa kwa Yahya, kocha Mromania, Aristica Cioaba amepewa jukumu la kusajili mshambuliaji mwingine.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC ‘YAMTUPIA VIRAGO’ RASTA MGHANA YAHYA MOHAMMED Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top