• HABARI MPYA

    Thursday, November 09, 2017

    TFF YAMPA POLE SAMATTA, YAMUOMBEA APONE MAPEMA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limempa pole na kumtakia kupona mapema Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta ambaye, atakosa mchezo kati Tanzania na Benin utakaofanyika Novemba 12, 2017 kwa sababu ya majeraha ya goti.
    Taarifa ya TFF Jumatano imesema kwamba Mbwana Samatta anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mdogo na mpaka kupona, madaktari wamesema itamchukua wiki nane ili kurejea uwanjani.
    Kocha wa Taifa Stars, Salum Shabani Mayanga amepokea taarifa hiyo na kusema haijawa bahati kwa Stars, lakini atapanga kikosi chake vema kwa wachezaji atakaokuwa huko Benin akiwamo Abdi Banda na Farid Mussa.
    Wachezaji watakaosafiri ni Aishi Manula, Peter Manyika, Gadiel Michael, Boniphas Maganga, Kelvin Yondani, Nurdin Chona, Himid Mao, Hamis Abdallah, Raphael Daudi, Mohamed Issa, Jonas Mkude, Mudathir Yahya, Simon Msuva, Shiza Kichuya, Faridi Mussa,  Ibrahim Ajib, Mbaraka Yusuph na Elias Maguli.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAMPA POLE SAMATTA, YAMUOMBEA APONE MAPEMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top