• HABARI MPYA

  Thursday, November 09, 2017

  REFA WA AZAM NA MBEYA CITY 'AENDA NA MAJI', AFUNGIWA MIEZI MITATU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  REFA Shakaile Ole Yanga Lai amefungiwa miezi mitatu kwa kushindwa kuumudu mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City wiki mbili zilizopita.
  Katika mechi hiyo namba 57, Azam FC ikishonda 1 -0, Shakaile anatuhumiwa kutoripoti na kuchukua hatua dhidi ya kitendo cha Kipa Owen Chaima wa Mbeya City kumpiga kofi mshambuliaji wa Azam FC. 
  Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imesema kiitendo cha Mwamuzi huyo ni ukiukaji wa Kanuni ya 38(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi wakati adhabu dhidi yake imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu.
  Naye Kamishna wa mechi hiyo, David Lugenge amefungiwa miezi mitatu kwa kushindwa kuripoti tukio hilo. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 39 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Kamishna.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: REFA WA AZAM NA MBEYA CITY 'AENDA NA MAJI', AFUNGIWA MIEZI MITATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top