• HABARI MPYA

  Thursday, November 09, 2017

  DAR CTY KUONYESHAA KAZI NA MAJI MAJI KOMBE LA AZAM

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MICHUANO ya Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC), inaendelea kesho Alhamisi Novemba 9, 2017 kwa michezo saba ambako Dar City itacheza  na Majimaji Rangers ya Lindi.
  Mchezo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Bandari jijini Dar es Salaam huku Real Mojamoja ya Iringa ikiwa wenyeji wa African Wanderers kwenye Uwanja wa Samora mkoani Iringa wakati Shupavu na Sabasaba zitachuana mjini Morogoro.
  Mashujaa ilikwisha kupata mpinzani ambaye ni Buseresere ambaye kabla aliifunga Isoko katika hatua ya awali. Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
  The Mighty Elephant itacheza na Makanyagio kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Namungo na Villa Squad nazo zinacheza kesho kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara .
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DAR CTY KUONYESHAA KAZI NA MAJI MAJI KOMBE LA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top