• HABARI MPYA

    Friday, November 10, 2017

    SABABU ZAIDI ZA NEYMAR KWENDA REAL MADRID HIZI HAPA

    UTABIRI wa kwamba nyota Neymar ataondoka Paris Saint-Germain kwenda Real Madrid umezidi kupewa nafasi, safari ikidaiwa mahusiano yasiyoridhisha na kocha Unai Emery yanaweza kuwa sababu. 
    Inaelezwa kwamba Emery amekuwa ni kocha mwenye historia ya msimamo mkali wa kinidhamu kwa wachezaji wake, ambaye hutaka wamsikilize na kufuata mafundisho yake kuelekea kwenye mechi. 
    Wasiwasi umeanza kuibuka kwamba Emery hataweza kuishi na Neymar kwa sababu ni mchezaji ambaye hatamudu kumpa maelekezo namna ya kuwapita mabeki keuelekea kwenye mechi. 
    Na kama mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa dau la rekodi ya dunia Paris Saint-Germain ataendelea kuwa mfalme wa klabu, wazi kocha huyo hatakuwa na furaha.
    Emery hajawahi kuwa na chumba cha kuvalia nguo chenye wachezaji ghali namna hiyo kabla na pia hawezi kuhoji chochote juu ya majukumu ya Neymar kwa sababu hakutwaa mataji ya Ligue 1 na Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.
    Baada ya matokeo hayo, mchezaji huyo wa ghali wa dunia ameletwa ili kuisaidia timu kushinda mataji.
    Lakini Emery anaona Neymar alikuwa tatizo katika kugombea kupiga penalti na Edinson Cavani. 
    Pia kuna tetesi kwamba msimu huu Neymar atatumika mno katika mechi za mashindano ya ndani, hivyo atahitaji kupumzishwa kabla ya Ligi ya Mabingwa na mechi za timu yake ya taiga. 
    Hawezi kushinda Ballon d'Or kwa kutwaa taji la Ligue 1, hanahitaji kushinda Kombe la Dunia na Ligi ya Mabingwa kwa ajili hiyo.
    Neymar (kushoto) akisalimiana na Cristiano Ronldo hivi karibuni PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

    TAKWIMU ZA NEYMAR KLABU YA PSG 2017/18

    Ligue 1 
    Mechi alizocheza: 8   Mabao aliyofunga: 7
    Pasi za mabao: 6
    Ligi ya Mabingwa
    Mechi alizocheza: 4   
    Mabao aliyofunga: 4
    Pasi za mabao: 3
    Huku PSG ikitarajiwa kutwaa ubingwa wa Ligue 1 bila kuvuja jasho, inafikiriwa Emery atakuwa katika wakati mgumu kwa sababu atashindwa kuwatazama wachezaji wengine kama yeye ndiye hatakuwa wa kuamua nani wa kupumzika na lini.
    Gazeti kubwa nchini Ufaransa, L'Equipe liliandika kwamba mahusiano baina ya Neymar na kocha  – na tofauti iliyoibuka mapema tu kati ya Neymar na Cavani, mwisho wa siku mshindi atakuwa mmoja tu.
    Cavani anacheza vizuri kwa sasa kuliko wakati wote na amekuwa mchezaji muhimu hata kwenye timu yake ya taifa kuelekea Fainali za Kombe la Dunia mwakani, tena zaidi ya mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez aliyeingia kwenye ukame wa mabao kwa sasa.
    Gazeti la Le Parisien liliandika mwezi uliopita kwamba Neymar anafurahia maisha kutokana na vipaumbele alivyowekewa katika klabu hiyo – ikiwemo kuwa na wataalamu wake mwenyewe wa kuyaweka maungo yake vizuri mjini Paris na si Rafael Martini au Ricardo Rosa anayemhudumia mchezaji mwingine yeyote. 
    Zlatan Ibrahimovic alikwenda na physio wake mwenyewe pia PSG.
    Neymar ni mchezaji pekee ambaye hasafiri na begi rasmi la timu, kwani ana mabegi yake maalum anayosafiri nayo. 
    Amepewa ruhusa maalum ya kutorudi nyuma wakati wa mechi na wachezaji wengine wameambiwa kutomuingia kwa nguvu mazoezini ili wasimuumize. 
    Haya yote ni kwa mujibu wa vyombo vya Habari nchini Ufaransa.
    Wakati huo hyuo tetesi za kwenda Real Madrid zimeibuka rasmi wiki hii kuhusu mchezaji huyo wa tatu kwa ubora duniani kwa sasa.
    Sergio Ramos alikuwa mwenye furaha kuzungumzia mchango wake. "Ningependa kuwa na mchezaji bora na ni wazi Neymar ni miongioni mwao.
    Inakumbushwa pia kwamba Real Madrid walimtaka Neymar alipokuwa mdogo katika klabu ya Santos ya nyumbani kwao na sasa Cristiano Ronaldo akiwa ana umri wa miaka 33 na msimu huu akiwa amefunga bao moja tu kwenye ligi hadi sasa kuna mahitaji makubwa ya kusajiliwa nyota mwingine.
    Madrid walitarajia Ronaldo angekwenda PSG msimu huu na wao wangetoa fedha kumsajili Neymar lakini klabu ya Paris ikaharibu mpango huo kwa kumuwahi Mbrazil huyo.
    "Labda ilikuwa rahisi kwake kwenda PSG, kuliko kuja moja kwa moja Real Madrid,"alisema Ramos katika mahojiano na kituo cha Redio nchini Hispania, Cadena Ser
    Neymar ambaye angepoteza haki zake zote Barcelona kama angehamia moja kwa moja Madrid, hadi sasa akiwa PSG amefunga mabao 11 katika mechi 12. 
    Pamoja na mwanzo huu mzuri katika miezi yake mitatu ya mwanzo, kuna uwezekano akaondoka PSG ikiwa Real Madrid na Manchester United zitaamau kuwania saini yake.
    Na hilo litawezekana kwa wepesi iwapo PSG hairafanya vizuri kwenye hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mapema 2018, kwani Neymar atakuwa na mzunguko wa pili mrefu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SABABU ZAIDI ZA NEYMAR KWENDA REAL MADRID HIZI HAPA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top