• HABARI MPYA

  Friday, November 10, 2017

  ERIC DIER NAHODHA ENGLAND IKIIVAA UJERUMANI LEO WEMBLEY

  Eric Dier atakuwa mchezaji wa sita kuvaa beji ya Unahodha wa timu ya taifa ya England chini ya kocha Gareth Southgate leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  MANAHODHA VIJANA WADOGO ENGLAND 

  Bobby Moore Miaka 22 na siku 47 v Czechoslovakia, 1963
  Michael Owen Miaka 22  na siku 125 v Paraguay, 2002
  Sol Campbell Miaka 23 na siku 254 v Ubelgiji, 1998
  Gerry Francis Miaka 23 na siku 272 v Uswisi, 1975
  Eric Dier Miaka 23 na siku 299 v Ujerumani, 2017
  Steven Gerrard Miaka 23 na siku 307 v Sweden, 2004
  Harry Kane Miaka 23  na siku 317 v Scotland, 2017
  NYOTA wa Tottenham Hotspur, Eric Dier atakuwa Nahodha wa sita wa England chini ya kocha 
  Gareth Southgate wakati atakapouiongoza timu yake ya taifa dhidi ya Ujerumani kwenye mchezo wa kirafiki leo.
  Huku Manodha wote wawili wa timu, Harry Kane na Jordan Henderson wakiwa nje kwa sababu ya majeruhi, Gary Cahill anasumbuliwa na maumivu ya mgongo na Joe Hart anatarajiwa kuanzia benchi, hivyo Dier atakuwa Nahodha wa England Uwanja wa Wembley Ijumaa.
  Huyo atakuwa mchezaji wa sita kuvaa kitambaa cha Unahodha wa timu ya taifa tangu Southgate achukue nafasi ya Sam Allardyce mwaka jana.
  Kane, Henderson, Cahill, Hart na Wayne Rooney wote wamekwishakuwa Manahodha wa England chini ya Southgate.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ERIC DIER NAHODHA ENGLAND IKIIVAA UJERUMANI LEO WEMBLEY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top