• HABARI MPYA

  Monday, November 21, 2016

  SIMBA YAITISHA MKUTANO WA MABADILIKO YA KATIBA WAMKABIDHI TIMU MO DEWJI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Utendaji ya Simba SC iliyokutana Novemba 18, Dar es Salaam imeitisha mkutano maalum kwa ajili ya mabadiliko ya Katiba utakaofanyika mwezi ujao Jijini.
  Taarifa ya Simba SC kwa vyombo vya Habari leo, imesema kwamba Mkutano huo utafanyika Desemba 11 katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Jeshi la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam. 
  “Kamati ya Utendaji imetumia mamlaka iliyopewa na Katiba ya Simba ibara ya 22 kifungu cha kwanza,”imesema taarifa hiyo na kuongeza;
  Mohamed 'Mo' Dewji anataka kununua asilia 51 ya hisa za Simba kwa Sh. Bilioni 20 

  “Nyaraka zote muhimu za mkutano huo zitakabidhiwa kwa wanachama kupitia matawi yao kwa mujibu wa matakwa ya katiba, ibara ya 22 kifungu cha nne cha katiba ya klabu,”imesema.
  Taarifa hiyo imesema Mkutano huo ni mwendelezo wa maazimio ya Mkutano Mkuu wa kawaida uliofanyika Julai 31, mwaka huu, ambao uliazimia kubadili mfumo wa uendeshwaji wa klabu na kuingia kwenye kuuza hisa.
  Na kwa ujumla wanachama waliafiki mpango wa kumuuzia asilimia 51 kwa Sh. Bilioni 20 mfanyabiashara Mohamed ‘Mo’ Dewji.
  Hata hivyo, Serikali iliingilia kati mpango huo kwa kumshauri Mo Dewji na mfanyabiashara mwenzake kijana mwenye asili ya Kiasi Yussuf Manji kuanzisha timu za kama mfanyabishara mwenzao, Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa kuliko kuzing'ang'ania Simba na Yanga.
  Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja aliagiza kwanza kusitishwa michakato yote inayoendelea ya kubadilisha umiliki wa timu kutoka kwa Wanachama kwenda katika umiliki wa hisa na ukodishwaji kwa Klabu za Simba na Yanga hadi kutakapofanyika marekebisho ya katiba zao.
  Alisema klabu hizo zinapaswa kurekebisha katiba zao kwanza kabla ya kufanya mabadiliko hayo kwa mujibu wa Sheria ya Baraza hilo na Kanuni za Msajili namba 442 Kanuni 11 kifungu kidogo cha (1-9).
  Na Simba SC inapiga hatua kuelekea kutimiza agizo la Serikali kwa kuitisha mkutano wa mabadiliko ya Katiba. Ikumbukwe Manji anataka kuikodisha Yanga kwa miaka 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAITISHA MKUTANO WA MABADILIKO YA KATIBA WAMKABIDHI TIMU MO DEWJI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top