• HABARI MPYA

  Monday, November 21, 2016

  TOTO AFRICANS YAITA KADHAA KUWAJARIBU, SHEKIONDO KUZIKWA KRSHO KOROGWE

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MENEJA wa Toto Africans ya Mwanza, Khalfan Ngassa ‘Babu’ amesema kwamba wataanza mazoezi Jumatano kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na siku hiyo wachezaji wapya watafanyiwa majaribio.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS -ONLINE leo kwa simu jana kutoka Mwanza, Ngassa alisema kwamba baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, waligundua mapungufu kadhaa kwenye kikosi chao na sasa wanajaribu kuyafanyia kazi.
  Khalfan Ngassa ‘Babu’ (kushoto) amesema Toto Africans itaanza mazoezi Jumatano kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 

  “Tuligundua mapungufu kadhaa kwenye baadhi ya nafasi, ikiwemo kipa, beki wa kulia, mabeki wa kati, kiungo mchezeshaji na mshambuliaji. Kwa hivyo tukaanza kumulika mulika huku na kule kutafuta vijana wa kuongeza kwenye hizo nafasi,”alisema.
  Kiungo huyo wa zamani wa Pamba ya Mwanza na Simba SC ya Dar es Salaam amesema amefanikiwa kupata vijana kadhaa ambao wametakiwa kufika mazoezini kuanzia Jumatano kufanyiwa majaribio.
  “Kimsingi tumekwishakubaliana na hao vijana waje mazoezini tuwaangalie, kwa hivyo baada ya kuwaangalia ndiyo tutajua kama tutawasajili au la,”alisema.
  Toto Africans ilimaliza mkiani mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya mzunguko wa kwanza ikizibeba timu nyingine 15 kutokana na kuambulia pointi 12 katika mechi zote 15.
  Dhahiri Toto wana kazi ya kufanya kuimarisha kikosi kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu, ili kukwepa kushuka daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TOTO AFRICANS YAITA KADHAA KUWAJARIBU, SHEKIONDO KUZIKWA KRSHO KOROGWE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top